Wananchi wakiwa katika dirisha la malipo katika Kituo cha Afya cha Nyamagana.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akikagua utekelezaji wa maagizo katika Kituo cha Afya Nyamagana Jijini Mwanza
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akiwa katika dirisha la malipo kukagua matumizi ya mfumo wa kielektroniki kama umefungwa katika Kituo cha Afya Nyamagana Jijini Mwanza
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukagua utekelezaji wa maagizo katika Kituo cha Afya Nyamagana Jijini Mwanza
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akizungumza katika uzinduzi wa mashindano ya Umiseta yaliyozinduliwa na Makamu wa Rais Samia Hassan Suluhu jana Jijini Mwanza.

……………………


NAIBU Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), Selemani Jafo amempongeza Mbunge wa Nyamagana na Viongozi wote wa Wilaya ya Nyamagana kwa kutekeleza maagizo ya serikali kwa maslahi mapana ya wananchi.

Mnamo mwezi Februari, mwaka huu Jafo alitembelea wilaya ya Nyamagana ambapo licha ya kuongea na watumishi alitembelea pia miradi ya maendeleo na kutoa maagizo mbalimbali.

Miongoni mwa miradi hiyo ni ujenzi wa barabara za lami zinazojengwa chini ya ufadhili wa Benki ya dunia pamoja na kukagua miundombinu na utoaji wa huduma katika kituo cha afya cha Nyamagana.

Katika ziara yake, alitoa maagizo mbalimbali ambayo alitaka yatekelezwe Kabla ya mwishoni mwa mwezi Juni mwaka huu.

Hata hivyo, jana baada ya kufanikisha zoezi la ufunguzi wa mashindano ya UMISETA yaliyozinduliwa rasmi na Makamu wa Rais mama Samia Suluhu Hassan, Jafo amefuatilia utekelezaji wa maagizo hayo na kukuta viongozi na watendaji wa jiji la Mwanza wametekeleza kwa kiwango cha kuridhisha.

Katika ujenzi wa barabara ijulikanayo kwa jina la Tilapia road, Jafo amekuta barabara ya lami imekamilika na kubakia maeneo madogo sana ya kuweka taa za barabarani.

Katika Kituo cha Afya cha Nyamagana, Naibu Waziri Jafo amekuta agizo la kuwekwa kwa mifumo ya kukusanya mapato kwa njia ya kielektroniki ukiwa umekamilika na mapato yameanza kuongezeka kutoka sh. milion 4 hadi Sh.milioni 10 kwa mwezi.

Mbali na hilo, pia amekuta wamekamilisha kutenga eneo Maalum kwa wagonjwa wa bima ambapo katika eneo hilo la bima mapato yameongezeka kutoka wastani wa Sh.milioni 6 hadi zaidi ya Sh.milioni 10 kwa mwezi.

Kufuatia utekelezaji huo, Jafo amewapongeza viongozi wote wa Nyamagana akiwemo Mkuu wa wilaya, Mbunge, madiwani pamoja na timu ya watendaji wa jiji la Mwanza huku akiwataka

watendaji hao kuchapa kazi ili kuleta maendeleo kwa wananchi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...