Jeshi la polisi limethibitisha kuungana na wadau wa soka mkoa wa Dar es Salaam katika kuhakikisha ulinzi na usalama wa wachezaji, viongozi, waamuzi, mashabiki na mali zao wakati wote wa mashindano ya Ndondo Cup 2017.

Kamisha msaidizi wa polisi (ACP) Philip Kalangi amesema, jeshi la polisi litatumia mbinu ya ulinzi shirikishi pamoja na wadau wengine wa vyombo vya ulinzi na usalama kuhakikisha amani inakuwepo wakati wote wa mashindano.
Kamisha msaidizi wa polisi (ACP) Philip Kalangi  akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na maandalizi ya kiusalama kwenye michuano ya Ndondo Cup inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Juni 17 mwaka huu ikiwa ni hatua ya mtoano.


“Tumejipanga lakini tutakuwa na ullinzi shirikishi ambao utahusisha wadau wengine wa vyombo vya ulinzi na usalama na vikundi mbalimbali vya ulinzi navyo vitakuwepo. Tunawasihi wananchi wajitokeze kwa wingi kuja kuona vijana wao, wapate burudani na mwisho wa siku tupate kitu tunachokitarajia.”

“Suala la ulinzi na usalama ni muhimu sana katika jambo lolote kwenye maisha ya kila siku, ulinzi na usalama ni suala mtambu na linahitaji ushirikishwaji wa pamoja, makuindi yote katika jamii yetu tunatakiwa tushiriki katika nafasi yake linahitaji kushiriki moja kwa moja katika ulinzi na usalama.”

“Hata kwenye jeshi la polisi tunafanya michezo, tuna program moja inaitwa michezo na vijana ambapo tumekuwa tunahamasisha vijana kuachana na matumizi ya madawa ya kulevya na uhalifu wa aina mbalimbali.

Mratibu wa michuano ya Ndondo Cup Shafii Dauda akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na maandalizi ya kiusalama kwenye michuano ya Ndondo Cup inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Juni 17 mwaka huu ikiwa ni hatua ya mtoano, kulia ni Kamisha msaidizi wa polisi (ACP) Philip Kalangi.

“Kama mnavyofahamu, michezo inajenga ushirikiano, upendo na mambo mengi lakini kubwa ni ajira. Vijana wengi hawana ajira kwa hiyo kwenye mashindano haya tunategemea vipaji mbalimbali vitaibuliwa na kuwasaidia hapo badae kwenye maisha yao.”

“Sisi kama jeshi la polisi tutakuwepo na tumekuwa na mahusiano na raia enzi na enzi tangu kuanzishwa kwa jeshi la poilisi, hauwezi kututenga na raia wala huwezi kuwatenga raia na askari. Kwa hiyo ushirikiano ni lazima uwepo na uendelee kwenye masuala ya ulinzi na usalama.” 

Michuano ya Ndondo Cup 2017 hatua ya makundi inataraji kuanza rasmi Jumamosi Juni 17, 2017 ambapo mechi ya ufunguzi wa hatua ya makundi itazikutanisha Stimtosha dhidi ya Makuburi kwenye uwanja wa Kinesi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...