NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
SHIRIKA la Umeme Nchini, (TANESCO), limewahakikishia watanzania kuwa mradi wa umeme wa gesi wa Kinyerezi II unaendelea kwa kasi kubwa na utakamilika kama ilivyopangwa.

Hakikisho hilo limetolewa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Dkt. Tito E. Mwinuka, wakati wa ziara yake ya kutembelea mradi wa umeme wa gesi wa Kinyerezi II jijini Dar es Salaam, ambao unatarajiwa kutoa Megawati 240 za umeme.

“Niwahakikishie watanzania kuwa ifikapo Agosti mwakani (2018), mradi wa umeme Kinyerezi II utakamilika na hivyo tutaongeza Megawati 240 kwenye gridi ya Taifa.” Alisema Dkt. Mwinuka wakati akitoa majumuisho ya ziara yake.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dkt. Tito E. Mwinuka (katikati), akiongozana na Meneja wa mradi wa upanuzi wa Kinyerezi I, Mhandisi Simon Jilima,(kushoto) na Meneja Mwandamizi wa Miradi wa TANESCO, Mhandisi Gregory Chegere, wakitembelea kukagua maendeleao ya ujenzi wa mradi wa Kinyerezi II na ule wa upanuzi wa Kinyerezi I jijini Dar es Salaam, leo Juni 17, 2017.

Sehemu ya mitambo hiyo.
DKT. Mwinuka, (kulia), Msaidizi wa Mkurugenzi Mtendaji anayeshughulikia miradi, Mhandisi Khalid James, (katikati) na Meenja Mradi wa Kinyerezi II, Mhandisi Stephen A.S.Manda, wakijadiliana jambo.
Mitambo ikiteremshwa eneo la ujenzi
Mkurugenzi wa Business Times, Imma Mbuguni, (kulia) akizungumza jambo na Mhandisi, Khalid James.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...