Na Karama Kenyunko,blogu ya jamii.

Julai 13, mwaka huu Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu imepanga kuanza kusikiliza kesi ya dawa za kulevya inayomkabili video Queen Agnes Gerald (28) maarufu kama Masogange.

hatua hiyo imekija baada upande wa mashtaka kukamilisha upelelezi na leo kumsomea mshtakwa maelezo ya awali (PH).

Katika Ph Hiyo Masogange amekiri kupelekwa kwa Mkemia Mkuu kuchukuliwa sampuli ya mkojo wake ili kuthibitisha kama anatumia dawa za kulevya.

Masogange amekubali hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri wakati Wakili wa Serikali, Costantine Kakula alipokuwa akimsomea maelezo ya awali ya mashitaka yake.

Pia Masogange amekiri kuwa Februari 14, mwaka huu alikamatwa nyumbani kwake Makongo juu Kinondoni Dar es Salaam na kupelekwa Kituo cha Polisi Central

Ikadaiwa kuwa, Februari 15, mwaka huu Masogange alipelekwa kwa mkemia kuchukuliwa sampuli zake.Aidha, alikiri kuwa na hati ya kusafiria yenye namba AB 783597.

Hata hivyo, Mshitakiwa huyo amekana kuwa Februari 20, mwaka huu Mkemia Mkuu alitoa taarifa iliyothibitisha kwamba mkojo wake ulikuwa na dawa aina ya heroin na Oxazepam.

Kufuatia hayo, kesi hiyo itaendelea Julai 13 mwaka huu ambapo upande wa mashtaka utaleta mashahidi wake.

Masogange anakabiliwa na mashitaka mawili ya kutumia dawa za kulevya aina ya heroin diacety na Oxazepam.

Inadaiwa kuwa, kati ya Februari 7 na 14 mwaka huu, maeneo yasiyofahamika jijini Dar es Salaam Masogange alitumia dawa za kulevya aina ya heroin (diacety/morpline) kinyume na sheria.

Aidha anadaiwa kutumia dawa za kulevya aina ya Oxazepam. 

Masogange yupo nje kwa dhamana.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...