Na Stella Kalinga, Simiyu
Shirika la Kidini la Madhebu ya Kikristo la Life Ministry limetoa vifaa tiba vyenye thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 40 kwa Hospitali Teule ya Mkoa wa Simiyu, Mjini Bariadi.
Akipokea vifaa hivyo Mkuu wa Mkoa huo, Mhe.  Anthony  Mtaka ameishukuru Life Ministry kwa msaada huo na kuwahakikishia kuwa vifaa hivyo vitasaidia kuboresha utoaji wa huduma za afya kwa wananchi katika hospitali hiyo.
Aidha, amesema Serikali iko tayari kushirikiana na madhehebu ya dini katika  kuhakikisha kuwa afya za wananchi zinakuwa salama, hivyo akawahakikishia kuwa  milango iko wazi kwa taasisi nyingine za dini zinazotaka kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuboresha huduma za afya.
Mtaka ameongeza kuwa ili Madaktari na wauguzi waweze kutekeleza majukumu yao vizuri ni lazima wawezeshwe vifaa, hivyo msaada huo utawatia moyo na kuongeza ari ya kufanya kazi.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Life Ministry hapa nchini, Dismas Shekalaghe amesema vifaa hivyo vimetolewa kama sehemu ya kuisaidia jamii ambavyo vitawawezesha madaktari na wauguzi kuwahudumia wananchi.
Shekalaghe ameongeza kuwa wao wanaamini kuwa ili mtu aweze kumtumikia Mungu  ni lazima awe na afya njema, hivyo kupitia msaada huo wa vifaa wagonjwa watahudumiwa na kurudi katika hali zao kawaida na kuendelea kumtumikia Mungu na kufanya shughuli za maendeleo.
 Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.  Anthony Mtaka(katikati), Mganga Mfawidhi wa Hospitali Teule ya Mkoa, Dkt. Fredrick Mlekwa(kushoto) wakipokea baadhi ya vifaa vilivyotolewa  Life Ministry kutoka kwa Mkurugenzi wa Shirika hilo la dini, Bw. Dismas Shekalaghe(Kulia).

 Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.  Anthony  Mtaka(katikati), Mganga Mfawidhi wa Hospitali Teule ya Mkoa, Dkt. Fredrick Mlekwa(kushoto) wakikabidhiwa viti vya kubebea wagonjwa na Mkurugenzi wa Life Ministry Bw. Dismas Shekalaghe (kulia).  ambavyo ni miongoni mwa vifaa vilivyotolewa  Shirika hilo la Kikristo kwa Hospitali Teule  ya Mkoa wa Simiyu.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...