THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Maadhimisho Siku ya Mtoto wa Afrika: Viongozi wa Dini Wakemea Ukatili


VIONGOZI wa Dini wamekemea vitendo vya ukatili kwa watoto na kwani vimekemewa hata katika vitabu vya dini, huku wakimtaka kila mmoja kumlinda mtoto pamoja na kueneza elimu ya malezi. Viongozi hao walioshiriki katika mkutano wa vyombo vya habari ulioandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA) kutoka Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) na Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) kwa pamoja waliungana na TAMWA kukemea vitendo vya kikatili wanaofanyiwa watoto, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika.

Akizungumza Mwakilishi kutoka Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA), Sheikh Shomari Mchongoma alisema jamii kwa pamoja inapaswa kuungana na kukemea vitendo vya kikatili kwani ni kinyume cha imani zetu. Alisema jambo pekee ambalo linaweza kufanikisha mapambano hayo ni jamii kumrudia mwenyezi Mungu na kukemea vitendo viovu anavyochukizwa navyo.

“…Wakati umefika tuangalie ni namna gani kumkomboa mtoto wetu kwenye wimbi la mateso ya kikatili ambayo wamekuwa wakitendewa baadhi ya watoto wetu. Mtoto anaweza kuwa salama endapo tutaungana na kukemea vitendo hivyo bila kujali tofauti zetu,” alisema Sheikh Mchongoma.

Kwa upande wake, Mwakilishi kutoka Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), Bw. Lucas Singili alisema mtoto anaitaji malezi ya pamoja kwa ushirikiano ikiwa ni kuwaweka karibu ili waweze kukua katika malezi mema. Watoto hawapaswi kutengwa wala kufanyiwa vitendo vya kikatili zaidi ya kuwapa msaada kutoka kwa wazazi, walezi na jamii kwa ujumla ili waweze kuwa raia wema wenye maadili katika taifa la baadaye.
Mwakilishi kutoka Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA), Sheikh Shomari Mchongoma (kushoto) akizungumza katika mkutano wa vyombo vya habari pamoja na viongozi wa dini kutoka BAKWATA, Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) na Mtaalamu wa Saikolojia ya Jamii, John Ambrose kukemea vitendo vya kikatili dhidi ya watoto, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika.
Ofisa Miradi wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA), Godfrida Jola (kulia) ambaye alimwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo akizungumza katika mkutano wa vyombo vya habari ulioandaliwa na kushirikisha viongozi wa dini kutoka Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) na Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) kukemea vitendo vya kikatili dhidi ya watoto, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika. Kutoka kushoto ni Sheikh Shomari Mchongoma (BAKWATA), Bw. Lucas Singili (CCT), pamoja na Mtaalamu wa Saikolojia ya Jamii, John Ambrose.
Mwakilishi kutoka Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), Bw. Lucas Singili (katikati) akizungumza katika mkutano wa pamoja na viongozi wa dini kutoka BAKWATA, CCT na Mtaalamu wa Saikolojia ya Jamii, John Ambrose kukemea vitendo vya kikatili dhidi ya watoto, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika. Mkutano huo uliandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA). Kulia ni Mtaalamu wa Saikolojia ya Jamii, John Ambrose na Sheikh Shomari Mchongoma wa BAKWATA (kushoto).