JESHI la polisi mkoa wa Iringa linamshikilia makamu mwenyekiti wa baraza la vijana la chama cha Demokrasi na maendeleo (BAVICHA ) Taifa Patrick Ole Sosopi (pichani) kwa tuhuma za kufanya mikutano ya hadhara bila kuwa na kibali cha jeshi la polisi . 
Akithibitisha hilo, Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Iringa John Kauga amesema kwamba  Sosopi alikamatwa leo asubuhi na kuwa bado jeshi hilo linaendelea kumshikilia kwa mahojiano kabla ya kufikishwa mahakamani kwa kosa la kufanya mikutano bila kibali cha jeshi hilo kwenye vijiji viwili vya Kinyika na Mlowa jimbo la Ismani wilaya ya Iringa mkoani hapa . 
 
Alisema kuwa makamu mwenyekiti huyo wa Bavicha alipewa kibali ya kufanya mikutano ya ndani ambayo inaruhusiwa ila hakufanya hivyo na badala yake kufanya mikutano ya nje kinyume na taratibu na kuwa mikutano hiyo ilifanyika kati ya tarehe 16 na 17 mwaka huu . 

Tunaendelea kumshikilia Sosopi kutokana na kosa la kuvunja sheria kwa kufanya mikutano ya hadhara pasipo kuwa na kibali cha polisi kimsingi mikutano yote ya hadhara kwa vyama vya siasa ilipigwa marufuku na mikutano inayoruhusiwa na ile ya ndani pekee ila yeye aliomba kibali cha kufanya mikutano ya ndani ila hakuweza kufanya hivyo na badala yake alifanya mikutano ya hadhara nje “ 
Hata hivyo kaimu kamanda huyo hakusema ni lini makamu mwenyekiti huyo wa BAVICHA Taifa atafikishwa mahakamani.

Hatua ya kukamatwa kwa Sosopi imekuja zikiwa zimepita wiki mbili toka aliposhikiliwa na kuachiwa kwa dhamana jeshi la polisi la polisi kwa tuhuma za kufanya mkutano katika eneo la wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu Kijiji cha Nyakavangala.
Huko  alikamatwa kwa agizo la mkuu wa wilaya ya Iringa Mhe. Richard Kasesela kwa madai ya kufanya mkutano huo  kutoa maneno ya uchochezi kwa wachimbaji hao

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...