Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amewasili mkoani Mara alasiri ya  jana Jumamosi  akitokea mkoani Mwanza ambapo leo  atakuwa  mgeni rasmi katika kilele cha Siku ya Mazingira Duniani.
Alipowasili kijijini Butiama, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amepokelewa na Viongozi wa vyama vya siasa na watendaji mbalimbali wa Serikali ambao wameongozwa na Mkuu wa mkoa wa Mara Dkt Charles Mlingwa pamoja na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira January Makamba.
Makamu wa Rais pia amepokea taarifa ya maendeleo ya mkoa wa Mara na amepata fursa ya kuwasha mshumaa na kuweka shada la maua katika kaburi la baba wa Taifa Hayati Julius Nyerere lililopo Mwitongo kijijini Butiama.
Leo Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan ataongoza mamia ya wananchi wa mkoa wa Mara na mikoa ya Jirani katika Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani ambapo kitaifa sherehe hizo zitafanyika katika kijiji cha Butiama mkoani Mara. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka shada la maua juu ya kaburi la Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere mara baada ya kuwasili Butiama ambapo atakuwa mgeni rasmi kwenye sherehe za siku ya mazingira Duniani ambazo Kitaifa zinafanyika Butiama mkoani Mara.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akitoa heshima mbele ya kaburi la Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere mara baada kuweka shada la maua. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye kikao cha kupokea taarifa ya mkoa wa Mara mara baada ya kuwasili Butiama kwenye makazi ya Hayati Baba wa Taifa.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...