Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea kitabu cha picha kutoka kwa
Kamishna wa Utalii Zanzibar Javed Jafferji wakati wa hafla ya futari iliyoambatana
na uzinduzi wa Jumuiya ya Watoa Huduma za Mafuta na Gesi Tanzania (ATOGS) jana
Jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akionyesha kitabu cha picha alichokabidhiwa
na Kamishna wa Utalii Zanzibar Javed Jafferji (kulia) wakati wa hafla ya futari
iliyoambatana na uzinduzi wa Jumuiya ya Watoa Huduma za Mafuta na Gesi Tanzania
(ATOGS) jana Jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo ambaye
pia alikuwa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue.
Mwanzilishi wa Jumuiya ya Watoa Huduma za Mafuta
na Gesi Tanzania (ATOGS), Bw. Abdulsamad Abdulrahim akitoa maelezo kuhusu
malengo ya jumuiya hiyo mbele ya mgeni rasmi Makamu Rais Mhe. Samia Suluhu
Hassan, wakati wa hafla ya futari iliyoambatana na uzinduzi rasmi wa Jumuiya
hiyo jana Jijini Dar es Salaam. Mwanzilishi huyo alitoa mchango wa shilingi
milioni 25 kama mtaji wa kuanzia wa ATOGS.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiomba dua wakati wa hafla ya futari
iliyoandaliwa na Jumuiya ya Watoa Huduma za Mafuta na Gesi Tanzania (ATOGS)
jana Jijini Dar es Salaam, Mwanzilishi wa Jumuiya ya Watoa Huduma za Mafuta na
Gesi Tanzania (ATOGS).Kutoka kulia ni Waziri wa Viwanda na Biashara Charles
Mwijage na Mwanzilishi wa Jumuiya hiyo Bw. Abdulsamad Abdulrahim.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa
katika picha ya pamoja na wajumbe wa Jumuiya ya Watoa Huduma ya Mafuta na Gesi
Tanzania (ATOGS) mara baada ya kumalizika kwa hafla ya futari iliyoambatana na
uzinduzi wa Jumuiya hiyo jana Jijini Dar es Salaam. Lengo la Jumuiya hiyo ni
kushirikiana na Serikali katika kuwahamasisha wazawa kujihusisha na masuala ya
gesi na mafuta ili kuongeza mnyororo wa katika sekta hiyo. Picha
na Frank Shija - MAELEZO
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...