THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) yaahidi kusaidia maendeleo ya soka

 Naibu Mhifadhi (Huduma za Shirika) wa Mamlaka ya  Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), Asangye N. Bangu (kushoto), akipeana mkono na Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa TFF wa Maendeleo ya Soka (TFDF), Derek Murusuri. Bw Bangu alizitembelea ofisi za TFDF ili kujadili maeneo mbalimbali ya ushirikiano kati ya Mamlaka yake na Mfuko huo. Mazungumzo hayo yalifanyika katika ofisi za TFDF zilizoko Mikocheni jijini Dar Es Salaam leo (28 June 2017).
Katika mazungumzo hayo, Bw Bangu ameahidi kushirikiana na Mfuko huo katika kuendeleza soka la Tanzania.
Timu ya Taifa ya vijana walio chini ya miaka 20 (U-20), Ngorongoro Heroes, inatumia jina la Mamlaka hiyo ya Taifa ambayo pia ni mojawapo ya maajabu saba ya dunia.