Mgeni rasmi katika Mashindano ya Kuhifadhi Qur-an, Waziri wa Nchi, Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mohamed Abood akimkabidhi zawadi mshindi wa maswali ya papo kwa papo, Ilham Idrisa (kulia). Kushoto ni Mdhamini ya mashindano hayo, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Mhandisi Hamad Masauni. Watatu kushoto, Mwakilishi wa Jimbo hilo, Nassor Salim Jazeera. Mashindano hayo yaliyoshirikisha Madrasa mbalimbali za Jimbo la Kikwajuni pamoja na maeneo mbalimbali ya Zanzibar na Tanzania Bara, yalifanyika katika Viwanja vya Mnara wa Kisonge mjini Unguja. Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Mhandisi Hamad Masauniakizungumza kabla ya mgeni rasmi katika Mashindano ya Kuhifadhi Qur-an, Waziri wa Nchi, Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mohamed Abood(katikati) kukabidhi zawadi kwa washindi wa mashindano hayo.Mashindano hayo yaliyoshirikisha Madrasa mbalimbali za Jimbo la Kikwajuni pamoja na maeneo mbalimbali ya Zanzibar na Tanzania Bara, yalifanyika katika Viwanja vya Mnara wa Kisonge mjini Unguja na kudhaminiwa na Mbunge wa Jimbo hilo. Kulia ni Mwakilishi wa Jimbo hilo, Nassor Salim Jazeera.

Mwanafunzi Khamis Mussaa kionyesha jitihada zake katika Mashindano ya kuhifadhi Qur-an katika Jimbo la Kikwajuni, Unguja, Zanzibar, linaloongozwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, na mdhamini wa mashindano hayo, Mhandisi Hamad Masauni (hayupo pichani). Mashindano hayo yalishirikisha Madrasa mbalimbali za Jimbo la Kikwajuni pamoja na maeneo mbalimbali ya Zanzibar na Tanzania Bara. 

Sehemu ya washiriki katikaMashindano ya Kuhifadhi Qur-an wakimsikiliza mdhamini wa Mashindano hayoNaibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Mhandisi Hamad Masauni (hayupo pichani), wakati nalipokua akitoa hotuba yake. Katika hotuba yake Masauni alisema washiriki wameonyesha uwezo mkubwa wa kuhifadhi Qur-an. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...