Mbunge
wa Viti Maalumu Bi Amina Mollel, akiwakabidhi msaada wa vitu Mbalimbali
Wanafunzi wenye mahitaji Maalumu wa Shule ya Msingi Buhangija iliyopo
mkoani Shinyanga, Sambamba na Msaada huo aliweza Kukabidhi Kadi za Bima
ya Afya Kwa ajili ya Matibabu.
Wanafunzi
wa Shule ya Msingi Buhangija Wakiwa wameketi, Wakati Mbunge wa Viti
Maalum Bi Amina Mollel alipofika Kwenye Kituo hicho Kukabidhi Misaada ya
Vitu Mbalimbali Ikiwemo Chakula na Kadi ya Bima ya Afya Kwa ajili ya
Matibabu Kwa Watoto hao.
Mbunge
wa Viti Maalum Bi Amina Mollel akipata Maelezo Mbalimbali Kutoka Mmoja
wa Viongozi wa Kituo cha Buhangija Kinachohudumia Watoto wenye Mahitaji
Maalum.
Watoto
wenye Albnism Wanaosoma Shule ya Msingi Buhangija iliyopo Mkoani
Shinyanga Wakimsikiliza Mbunge wa Viti Maalum Bi Amina Mollel, aliyefika
Kwenye Kituo Hicho Kuwapatia Msaada wa Vitu Mbalimbali ikiwemo Kadi za
Bima ya Afya Katika Mwezi Huu Mtukufu wa Ramadhani.
Mbunge
wa Viti Maalum Bi Amina Mollel akizungumza na Baadhi ya Viongozi pamoja
na Walimu Katika Shule ya Msingi ya Buhangija iliyopo Mkoani Shinyanga,
Baada ya Kukabidhi Msaada wa Vitu Mbalimbali pamoja na Kadi za Bima ya
Afya Kwa ajili ya Matibabu Kwa Watoto wenye Mahitaji Maalum.
Walimu
wa Shule ya Msingi ya Buhangija Wakiwa Katika Picha ya Pamoja na Mbunge
wa Viti Maalum Bi Amina Mollel ambae alifika Kwenye Shule hiyo Kwa
ajili ya Kutoa Msaada Kwa Watoto wenye Mahitaji Maalum.
Picha kwa Hisani ya www.habari360.co.tz
Picha kwa Hisani ya www.habari360.co.tz
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...