VICTOR MASANGU, KIBAHA

VIJANA wa dini ya kiislmamu hapa nchini wametakiwa kuachana na vitendo vya kushinda vijiweni na kujiingiza katika wimbi la uhalifu na utumiaji wa madawa ya kulevya ambayo yanachgangia kwa kisi kikubwa kupoteza nguvu kazi ya Taifa na badala yake sasa wawe wazalendo kwa kuhakikisha wanazilinda kwa hali na mali rasilimali zote pamoja na kutunza amani iliyopo

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Sheikh wa Mkoa wa Pwani Hamisi Mtupa wakati wa sherehe za baraza kuu la waislamu la Iddy ngazi ya Wilaya ya Kibaha ambalo limefanyika katika viwanja vya mwendapole na kuhudhuliwa na viongozi wa ngazi mbali mbali wa dini pamoja na serikali kutoka katika Mkoa wa Pwani.

Sheikh Mtupa mbaye pia ni Kadhi wa Mkoa wa Pwani alibainisha kuwa kwa sasa watanzania wote wanapaswa kubadilika na kuhakikisha kwamba wanakuwa walinzi wa rasilimali zote zilizopo nchini kwa lengo la kuweza kuwathibiti baadhi ya watu ambao wamekuwa wakijinufaisha wao wenyewe kwa maslani yao binafsi bila ya kujali wananchi wa hali ya chini.

Hama kwa upande wake Mbunge wa jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka ambaye alikuwa mgeni rasmi katika sherehe hizo amewaasa wananchi wote kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Rais Dk John Magufuli pamoja na kuchapa kazi kwa bidii ili kuweza kupambana na janga la umasikini na kuachana na kuwa tegemezi ambapo pia amechangia kiais cha shilingi milioni tatu kwa ajili ya ujenzi wa ofisi ya waislmau ya Wilaya.

Koka alisesema kwamba nia yake kubwa ni kushirikiana na wananchi wa jimbo lake katika kuleta maendeleo hivyo amewaomba waislamu waendelee kujenga upendo na ushirikiano wa hali na mali katika kuakikisha kwamba ujenzi wa ofisi hiyo ya wilaya inakamilika ili iweze kuanza kufanya kazi kwa jili ya kutoa huduma.

“Mimi kama mbunge wenu katika hili kwa kuanzia nitachangia kiais cha shilingi milioni tatu lakini sio kwamba ndio nitaishia hapo hapana nataka kuona na nyinyi wenzangu tunashirikiana kwa pamoja ili kuweza kukamilisha ujenzi wa ofisi ya Wilaya na nikiona kwamba tupo pamoja na mimi tena nitaongezea kiasi cha shilingi milioni mbili lengo ikiwa ni kuona tunakuwa na sehemu sahihi ya kuweza kukutana na kufanya shughuli zenu,”alisema Koka.

Awali akisoma risala katika sherehe hizo Katibu wa kamati ya maandalizi ya Baraza la Iddi Wilaya ya Kibaha Hoseni Ibrahimu ameiomba serikali ya awamu ya tano kuongeza vipindi vya dini mashuleni kwa lengo la kuweza kutoa huduma za kiroho kwa wanafunzi wa kiislamu

“sisi kama baraza kuu la waislmamu Bakwata Wilaya ya Kibaha kikubwa tunachoiomba serikali ni kuongeza vipindi vingi vya dini katika mashule ili wanafunzi waweze kupata fursa ya kujifunza zaidi mafundisho ya kiroho na tuna imani itaweza kusaidia kuwaongezea uwezo mkubwa katika kujifunza mambo mbali mbali yanayohusina na dini ya kiislamu,”alisema Ibrahimu.


BARAZA kuu la waislamu (BAKWATA) Wilaya ya Kibaha Mkoa wa Pwani kwa sasa licha ya kukabiliwa na changamoto mbali mbali linahitaji kiasi cha shilingi milioni 15 kwa ajili ya kuanza maandalizi ya ujenzi wa ofisi ya wilaya.
Mbunge wa jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka akizungumza na waumini wa dini ya kiislamu hawapo pichani wakati wa sherehe za Baraza kuu la waislamu (BAKWATA) Wilaya ya Kibaha kwenye viwanja wa Mwendapole Wilayani Kibaha (PICHA NA VICTOR MASANGU) Caption-4 Naibu Sheikh wa Mkoa wa Pwani Hamisi Mtupa akizungumza jambo wakati wa sherehe hizo za baraza kuu la waislamu Wilaya ya Kibaha.(PICHA NA VICTOR MASANGU)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...