MKOA wa Singida umebuni mkakati wa kuanzisha dawati la sekta binafsi litakalokuwa chini ya afisa Maendeleo ya jamii wa Mkoa litakalotambua takwimu, mahali, aina ya shughuli na hali ya uzalishaji ili kuhakikisha ushiriki mtambuka unaowajibika ipasavyo kwa kumjulisha afisa ugani kuhusu uhitaji wa huduma za ugani kwa wajasiriamali.

Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk. Rehema Nchimbi alitoa kauli hiyo katika Kijiji cha Sanza wilayani hapa wakati alipokuwa akitoa salamu za Mkoa kwa Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa mwaka huu, Amour Hamad Amour.
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa uhuru kitaifa mwaka ahuu 2017,Bwana Amour Hamad Amour(wa tatu kutoka kushoto) akijiandaa kuukabidhi mwenge huo kwa kaimu Mkuu wa wilaya ya Manyoni, Miraji Mtaturu (hayupo pichani).

Aidha Mkuu wa Mkoa huyo wa Singida hata hivyo alizitaja shughuli zitakazovyafanywa na dawati hilo kuwa ni pamoja na kumjulisha Afisa ugani kuhusu uhitaji wa huduma za ugani kwa wajasiriamali pamoja na kutoa taarifa ya soko kwa mazao mbali mbali. Shughuli zingine kwa mujibu wa Dk.Nchimbi ni pamoja na kuwajulisha wafugaji tahadhari ya mlipuko wa magonjwa  na kufikisha kwa wanufaika fursa za kiuchumi zilizopo na hivyo kuifanya serikali kuwa bega kwa bega na sekta binafsi.

Hata hivyo Dk.Nchimbi aliweka bayana kwamba lengo la Mkoa ni kuwa na pikipiki zaidi ya saba kabla ya kilele cha mbio za Mwenge Oktoba, 2017 wataakuwa wamepata pikipiki hizo na kumuahidi kiongozi huyo mkuu wa mwenge kwamba atamtumia taarifa ya uthibitisho popote atakapokuwa.
 
Aidha Mkuu huyo wa Mkoa aliutaja mkakati wa pili katika ubunifu huo wa Mkoa kuwa ni kuwapa mizinga ya nyuki kwa shughuli mbadala kwa wachoma mkaa. “Wachoma mkaa hawa wanakiri kuwa kufuga nyuki siyo tu kunaokoa mazingira na raslimali bali ni hakikisho la wao kushiriki vema katika kukuza uchumi wa viwanda na maendeleo ya Mkoa na nchi kwa ujumla”alifafanua. Hata hivyo aliweka bayana kwamba mizinga wanayopewa itaambatana na elimu ya mara kwa mara na kwamba mradi wa kuashiria mkakati huo wa “ACHIA SHOKA KAMATA MZINGA” utakutwa wilaya ya Mkalama.

Naye Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa mwaka huu wa 2017, Amour Hamoud Amour akizungumza na wananchi wa Mkoa wa Singida wakati alipokuwa akiuaga msafara wa mbio za mwenge wa uhuru kutoka Mkoa wa Dodoma, alionyesha kuridhishwa na jinsi watendaji pamoja na wananchi wa Mkoa wa Dodoma kwa namna walivyouenzi mwenge huo. 

Mwenge  wa uhuru kitaifa mwaka huu wa 2017 wenye kauli mbiu isemayo “SHIRIKI KUKUZA UCHUMI WA VIWANDA VYA NCHI YETU”umeanza mbio zake Mkoani Singida baada ya kumaliza mbio zake Mkoani Dodoma ambapo utakapokuwa mkoani Singida,miradi yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 21.9,ikiwemo miradi 14 itafunguliwa,utazindua miradi 8,utaweka mawe ya msingi miradi 13 na utatembelea miradi 10.
baadhi ya viongozi wa chama na serikali wa wilaya ya Manyoni wakijiandaa kupokea mwenge wa uhuru kutoka kwa kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa mwaka huu wa 2017, Amour Hamad Amour.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...