Shirika la ActionAid-Tanzania, Mtandao wa Elimu Tanzania, Shirika la Maendeleo ya Elimu Singida-MEDO na Mtandao wa Asasi za Kiraia-KINGONET  kwa pamoja wanatekeleza mradi wa uhamasishaji utoaji elimu bora kupitia rasilmali zetu wenyewe ( PROMOTING QUALITY EDUCATION THROUGH PROGRESSIVE DOMESTIC RESOURCE MOBILIZATION) unaotekelezwa huko Kilwa na Singida Vijijini kwa ngazi ya wilaya kwa kufanya kazi na kamati za shule na klabu za haki za watoto shuleni.

 Kitaifa MRADI Huo unalenga kufanya  utetezi wa mabadiliko ya kisera na sheria  hasa suala la ulipaji kodi, ukusanyaji kodi kwa haki (tax Justice), uzibaji wa mianya ya uvujaji wa kodi  ili makusanyo yaongezeke na yagharimie huduma bora kwa wananchi wa Tanzania hususani kuboresha utoaji wa Elimu bora Nchini.

Mratibu wa Mtandao wa Elimu Tanzania Bi. Cathleen Sekwao akifungua mkutano huo aligusia pia kuhusu “utoaji wa huduma za jamii hapa nchini unakabiliwa na ufinyu wa fedha, wote tu mashahidi kuwa hadi kufikia mwezi Machi, 2017 serikali ilikuwa imetoa asilimia 34 tu ya bajeti yote ya 2016/2017. 

 Jambo hili lina madhara makubwa katika utoaji wa huduma za jamii hasa elimu msingi yenye ubora  hasakwa mtoto wa kike”.
Aliongelea pia serikali kushindwa kutoa asilimia mia moja ya fedha za kutekeleza bajeti ya 2016/2017 tafiti zinaonyesha kuwa Tanzania inapoteza fedha nyingi kupitia misamaha ya kodi.
Mwakilishi kutoka Mtandao wa Kodi Tanzania (TTJC), Grace Masalakulangwa akiwasilisha ripoti ya utafiti ya One Billion Question iliyotafitiwa na shirika la ISCEJIE katika Mkutano uliowakutanisha wadau wa Elimu na Wenyeviti wa Chama cha Walimu ngazi ya mikoa ya Tanzania Bara  iliyofanyika jijini  Dar es Salaam. 
Afisa Mradi wa Elimu kutoka TENMET, Alistidia Kamugisha akifungua mkutano na kuwaelezea malengo ya mkutano huo wa siku mbili kwa wadau wa elimu na Chama cha Walimu Tanzania uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Blue Pearl jijini Dar es Salaam.
 Mratibu wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TENMET), Cathleen Sekwao akitoa mada kuhusu umuhimu wa ukusanyaji wa rasilimali za ndani na kuwekeza katika kuboresha sekta ya elimu hususani kwa mtoto wa kike na maslahi ya walimu katika mkutano uliowakutanisha wanachama wa chama cha walimu Tanzania (CWT/TTU).

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...