Na Mwandishi Wetu
Mwanasiasa mkongwe nchini Augustine Lyatonga Mrema amesema Rais John Pombe
Magufuli ameweka historia ya mapambano ya uchumi nchini kutokana na namna
ambavyo analishughulikia suala la madini.
Bwana Mrema amesema kuwa kitendo cha Mwenyekiti wa Kampuni ya Barrick Gold
Cooperation Profesa John Thornton kusafiri usiku kucha kuja kuonana na Rais Magufuli
na kukubali kuilipa Tanzania fedha zote ilizokoseshwa na Kampuni Acacia ni kielelezo
kuwa sio tu kuwa ujumbe wake umefika lakini zaidi inadhihirisha kuwa madai yake dhidi
ya kampuni hiyo ya uchimbaji madini ni ya msingi.
“Ni kiongozi gani barani Afrika aliyethubutu kuishutumu kampuni ya nje kama
alivyofanya Rais Magufuli halafu viongozi wake wakasafiri kuonana na kiongozi huyo
kutaka suluhu kama alivyofanya Mwenyekiti huyo wa Barrick kwa Tanzania?”alihoji
Bwana Mrema.
Mwanasiasa huyo aliungana na wito wa Rais Magufuli wa kuwataka baadhi ya watu
wanaowahusisha viongozi wastaafu na taarifa za Tume za Rais za kuchunguza
Makinikia.
“Si vizuri na kwamba si sheria kwa mtu yeyote kuwatukana au kuwashambulia marais
wastaafu kama ilivyo kwa Rais aliye maradakani na sheria inatoa dhabu kali kwa
wanaofanya hivyo” alieleza bwana Mrema.
BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI
BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...