THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

Mshindi wa Milioni 20 Arusha akabidhiwa mzigo wake

WAENDESHAJI wa Bahati Nasibu ya Biko, ‘Ijue Nguvu ya Buku, jana wamemkabidhi zawadi yake jumla ya Sh Milioni 20 mshindi wao wa Arusha, Oscar Haule, huku wakijigamba kufanikiwa kwa kiasi kikubwa kuwakwamua washiriki wao kwa kuwapa fedha zao haraka ili waziingize katika majukumu yao ya kiuchumi.

Mbali na kumpa zawadi hiyo ya fedha taslimu mshindi huyo, Biko pia wametangaza kutoa jumla ya Sh Milioni 500 kwa washindi wao waliocheza Biko mwezi Mei.

Akizungumza katika makabidhiano hayo, Mkurugenzi wa Biko Tanzania, Charles Mgeta, alisema wanaamini kuwa kiasi cha pesa walichompa mshindi wao atazitumia vizuri katika kujiletea maendeleo kama ilivyokuwa dhamira ya kucheza Biko na kufikia kutoa Sh Milioni 500 kwa washindi wa mwezi Mei.

“Tunampongeza Haule kwa kushinda donge nono la Sh Milioni 20 kutoka Biko katika droo iliyochezeshwa juzi Jumatano, sambamba na kuwapongeza wote wanaocheza mchezo huu kwa njia ya ujumbe wa maandishi kwa simu zao za Tigo, Vodacom na Airtel kwa kufanya miamala kwenye simu zao kwa kuingiza namba ya kampuni ambayo ni 505050 na ile ya kumbukumbu ikiwa ni 2456,” Alisema Mgeta.


Naye Balozi wa Biko, Kajala Masanja alisema mchezo wa Biko ni rahisi kucheza pamoja na kushinda, hivyo kila Mtanzania anapaswa kuanza kucheza ili aweze kuibuka na ushindi wa zawadi za papo kwa hapo kuanzia Sh 5000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni moja, huku zawadi nono ya droo kubwa ya Jumapili hii ikiwa ni Sh Milioni 20 kama ilivyokuwa Jumatano iliyopita.

“Huu ni wakati wakutajirika kwa kupitia Biko Tanzania ambapo hakuna bahati nasibu inayolipa haraka kama Biko, hivyo Watanzania wanapaswa kutumia vyema fursa za uwapo wa bahati nasibu hii iliyojizolea umaarufu nchini,” Alisema Kajala.


Mshindi wa Sh Milioni 20 wa Biko Oscar Haule mwenye fulana nyekundu akipokea hundi yake ya ushindi kutoka kwa Balozi wa Biko, Kajala Masanja.

Mkurugenzi Mtendaji wa Biko Tanzania, Charles Mgeta kulia akiwa katika picha ya pamoja na mshindi wa Milioni 20 wa Biko droo ya Jumatano Oscar Haule wa jijini Arusha mwenye fulana nyekundu.