THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

NAIBU WAZIRI ANTHONY MAVUNDE AKUTANA NA BALOZI WA USWISI NCHINI TANZANIA MJINI DODOMA


Naibu waziri wa Kazi,Vijana ,Ajira na Watu wenye Ulemavu Ndg. Anthony Mavunde leo amefanya mazungumzo na Balozi wa Uswisi Mh Florence Mattli katika ofisi za Wizara ya Kazi,Vijana,Ajira na Watu wenye Ulemavu mjini Dodoma juu ya namna bora ya ushirikiano kati ya Tanzania na Uswisi katika eneo la Ukuzaji Ujuzi kwa Vijana kupitia mpango unaotekelezwa na Wizara.

Balozi Mattli ameupongeza mpango wa Wizara wa utekelezaji wa Program ya Ukuzaji Ujuzi kwa Vijana nchini kupitia mafunzo stadi ambayo yana lengo la kuwajengea Vijana wa Tanzania ujuzi stahiki na hivyo kuwawezesha kuwa na sifa za kuajiriwa,Kujiajiri na kuajiri Vijana wengine.

Balozi Mattli ameahidi kushirikiana na Serikali katika kuunga mkono juhudi za Wizara katika uendeshaji wa Mafunzo ya Ufundi kwa Vijana kwa kufadhili kiasi cha Shilingi 34,000,000 USD kwa miaka 12 kwa ajili ya utekelezaji bora wa Mpango wa Ukuzaji Ujuzi kwa Vijana nchini.