THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

NHIF YAWANOA WAHARIRI WA VYOMBO VYA HABARI NCHINI, MJINI MOROGORO LEO

Katibu Tawala mkoa wa Morogoro, Clifford Tandari aliyesimama, akizungumza na wahariri na waandishi wa Habari katika warsha ya siku moja iliyoandaliwa na mfuko wa Bima ya Afya nchini, NHIF. Katika warsha hiyo, NHIF imepokea taarifa ya utafiti uliofanywa kwa ushirikiano na wanahabari kuangalia ubora/changamoto za utoaji wa bima ya afya nchini.
Kushoto kwake ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF Bernard Konga, Agnes Chaki, wa kwanza kushoto, na kulia kwake ni Mwenyekiti wa Jukwaa la wahariri Theophil Makunga na karibu wake, Nevil Meena. Picha na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii.
⁠⁠⁠Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Bima ya Afya nchini, NHIF, Bernard Konga akiongea na wahariri na waandishi wa Habari wakati wa warsha ya siku moja ya kupokea taarifa ya utafiti juu ya kuangalia ubora/ changamoto za utoaji wa bima ya afya nchini
Mkurugenzi msaidizi Habari maelezo, (Habari) Rodney Thadeus akiongea kwa niaba ya Serikali juu ya huduma zinazofanywa na NHIF nchini wakati ya warsha hiyo.
Baadhi ya wahariri wa nyombo mbalimbali vya habari nchini wakifuatilia warsha ya siku moja ya wanahabari iliyofanyikoa mkoani Morogoro, wakati NHIF ikipokea taarifa ya utafiti uliofanywa na baadhi ya waandishi wa Habari kuangalia ubora/ changamoto za utoaji wa bima ya afya nchini.
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia warsha hiyo.