Rais wa Special Olympics Kanda ya Afrika ambaye pia ni
mtendaji mkuu Bw. Charles Nyambe (pichani) anatarajia kufanya
ziara nchini Tanzania kuanzia tarehe 5/6/2017 hadi 9/5/2017.
Kwa mujibu wa Charles
Rays, Mkurugenzi Special Olympics Tanzania, akiwa Tanzania Bw. Nyambe atapata fursa ya kuendesha mafunzo ya uongozi wa michezo ya Special
Olympics kwa makocha 50, ambao ni waratibu wa mikoa yote 30, pamoja na
wengine 20 kutoka Dar es Salaam.
"Amependekeza pia kutumia masaa matatu kati ya siku nne
atakazokuwa nasi hapa Tanzania kukutana na kuendesha mafunzo ya uongozi kwa wajumbe wote wa board ya Special Olympics
Tanzania", amesema Bw. Rays.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...