Mkuu wa mkoa wa
Tanga Mh. Martine Shigella amewataka wahitimu wa mafunzo ya awali ya kijeshi ya vijana operasheni
Magufuli awamu ya pili wa kujitolea kutumia mafunzo waliyoyapata kwa kuwa
wazalendo na kufanya kazi kwa niaba ya Taifa la Tanzania.
Hayo ameyazungumza
wakati alipokuwa akifunga mafunzo ya kumaliza mafunzo ya awali ya kijeshi ya
vijana operesheni Magufuli awamu ya pili
wa kujitolea yaliyofanyika kwenye
Kituo namba 835KJ Mgambo JKT kilichopo Kata ya Kabuku Wilayani Handeni.
Mkuu wa Mkoa
amesema kuwa mafunzo ya ukakamavu wa mwili, uzalishaji mali, masuala mazima ya
ulinzi na usalama na mafunzo ya kijeshi yatumike kwa uzalendo na kuwa mfano
bora kwa jamii itanayowazunguka.
“ Nendeni mkawe
mfano bora wa kuigwa kwenye familia zenu
na wazazi wenu wamekuja hapa kuwashuhudia, Sisi kama Serikali tunawaamini”
alisema Shigella.
Ameongeza kuwa Mh.
Rais alipoamua kurudisha mafunzo haya alitambua umuhimu mkubwa kwa Taifa letu
sababu anajua mahitaji ya sasa na ya baadae wakati lengo kuu likiwa ni kuleta
usawa na uzalendo kwa wasomi na wasio wasomi.
Amewataka
wakatimize wajibu wao wa kuwa raia wema na kuwa walinzi wa Taifa kwa kupitia
mafunzo ya ulinzi na usalama waliyoyapata huku akieleza kuwa Serikali
inapambana na changamoto za kukabiliana na wahalifu ambao hawataki kuwa kama wanadamu wengine.
“ Nina imani kubwa na nyinyi kwamba mtaendelea
kuwa waadilifu, waaminifu na kuendelea kupiga vita vitendo vya rushwa na
ubadhilifu wa mali za umma na kwamba mtakuwa kimbilio la wanyonge na watu wenye
matatizo makubwa” alisema Shigella.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mh Martin Shigella akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo.
Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh Godwin Gondwe akizungumza wakati wa kufunga Mafunzo hayo.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mh Martin Shigella akitoka kukagua gwaride.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...