Waziri wa Kazi, Ajira, Sera, Bunge, Vijana na wenye ulemavu, Jenista Mhagama (alieshika panga) akikata muwa kuashiria uzinduzi uzinduzi wa mpango maalumu wa uwezeshaji wa wakulima wa miwa wa nje (Outgrowers scheme) katika mradi wa sukari wa Mkulazi wakati wa hafla ya uzinduzi iliyofanyika mkoni Morogoro mwishoni mwa wiki.Anaeshuhudia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Mkulazi ambae pia ni Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Prof Godius Kahyarara (kulia) pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bw.William Erio (kushoto).

Na Mwandishi wetu,

SERIKALI imesema uamuzi uliofanywa na Mifuko ya Hifadhi ya jamii wa kuwekeza kwenye sekta viwanda hapa nchini ni uamuzi sahihi huku ikitoa wito kwa wanachama na wadau wa mifuko kushiriki kikamilifu katika kutumia fursa zitokanazo na miradi hiyo.

Kauli hiyo ya Serikali imetolewa na Waziri wa Kazi, Ajira, Sera, Bunge, Vijana na wenye ulemavu, Jenista Mhagama  wakati akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa mpango maalumu wa uwezeshaji wa wakulima wa miwa wa nje (Outgrowers scheme) katika mradi wa Mkulazi iliyofanyika mkoni Morogoro mwishoni mwa wiki chini ya uratibu wa Kampuni  Hodhi ya Mkulazi Holding Ltd ambayo imetokana na na ubia kati ya mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya NSSF na PPF.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Bw Charles Mwijage (alieshika panga)akikata muwa kwenye uzinduzi huo.Anaeshuhudia ni Waziri wa Kazi, Ajira, Sera, Bunge, Vijana na wenye ulemavu, Jenista Mhagama (kushoto) na Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Mkulazi ambae pia ni Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Prof Godius Kahyarara (kulia).

Mpango huo mpya sehemu ni utekelezaji wa mradi mkubwa wa ujenzi wa kiwanda cha sukari kitakachojengwa na kwa ubia wa mifuko hiyo miwili katika eneo la Mkulazi, mkoani Morogoro na unalenga kuwashirikisha wakulima wa (outgrowers scheme)katika kilimo cha miwa kwa kiasi kikubwa ukuanzia na wananchi wa mkoa wa morogoro na Pwani.

 “Mbali na kuipongeza mifuko yetu ya Hifadhi ya Jamii kwa uwekezaji huu wenye tija kwa taifa naomba niwasihii sana msikatishwe tamaa na maneno ya watu yanayolenga kupotosha dhana nzima ya uamuzi huu makini lakini nataka niwathibitishie kuwa hadi sasa tupo kwenye mstari sahihi na dalili njema zimeanza kuonekana,’’ alisema.

 “Mpango huu licha ya kutengeneza ajira kwa watu zaidi ya 10,000 pia utapunguza na kuondoa kabisa tatizo la upungufu wa sukari nchini, kuzuia na kupunguza makali ya mfumuko wa bei kwa kuhakikisha bei ya sukari inaendana na gharama za uzalishaji,’’ aliongeza.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dk Steven Kebwe (alieshika panga) akikata muwa kwenye hafla ya uzinduzi huo.Anaeshuhudia ni Waziri wa Kazi, Ajira, Sera, Bunge, Vijana na wenye ulemavu, Jenista Mhagama pamoja na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Bw Charles Mwijage.

Kwa upande wake Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Bw Charles Mwijage mbali na kuipongeza mifuko hiyo kwa utekelezaji wa  mradi huo mkubwa pia aliongeza kuwa licha ya uwekezaji huo kuhusisha pia kilimo cha mazao mengine ikiwemo mpunga, alizeti, mahindi na mtama pia kuna haja ya kuhakikisha unahusisha uwekezaji katika sekta ya maziwa hoja iliyongwa mkono pia na Waziri Mhagama.

“Pamoja na pongezi zangu ninaomba mradi huu pia uhusishe uzalishaji wa maziwa kwa kuwa tunatarajia kupata mabaki mengi yatokanayo na mazao ambayo yanaweza kugeuka kuwa chakula cha mifugo,’’ alishauri.

Awali wakizungumzia mradi huo, Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Mkulazi ambae pia ni Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Prof Godius Kahyarara pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bw.William Erio, walihakikishia serikali, wananchama na wadau wote wa mifuko hiyo kuwa utekelezaji wa mpango huo unahusisha  uadilifu na uwazi ili kuleta matokeo chanya.
ZAWADI! Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Mkulazi ambae pia ni Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Prof Godius Kahyarara (kushoto) akimkabidhi zawadi Waziri wa Kazi, Ajira, Sera, Bunge, Vijana na wenye ulemavu, Jenista Mhagama (kwa kutambua mchango wake kwenye mradi huo. Wanaoshuhudia ni pamoja na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Bw Charles Mwijage pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dk Steven Kebwe, baadhi ya wabunge wa mkoa wa Morogoro pamoja na muwakilishi kutoka Gereza la Mbigili lililopo mkoani humo.

 “Tunajitahidi sana kuzuia kashfa yoyote katika utekelezaji wa mradi huu ili tusiitie doa nia njema ya Mheshimiwa  Rais lakini pia kuhakikisha kwamba fedha za wanachama wa NSSF na PPF zinabaki kuwa sehemu salama,’’ alisema Prof Kahyarara.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...