THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Sheikh Shariff afanya Dua maalum ya kuaga mwezi mtukufu wa Ramadhani jijini Arusha Sheikh Shariff Majini kutoka Dar es salaam Siku ya Eid Pili akiwa Arusha ameendesha Dua maalum ya kuaga Mwezi mtukufu wa Ramadhani. Sheikh aliifanya Dua hiyo katika viwanja vya soko la Kilombero stendi ya Hiace.
Dua ya Sheikh ilianza saa nane na kumalizika saa kumi na mbili jioni na kuhudhuriwa na wakazi wengi wa Jiji la Arusha. Pia Sheikh alipata nafasi ya kusikiliza shida mbalimbali za watu waliojitokeza katika Dua. Sheikh anataraji kuendelea na Dua Jijini Arusha siku ya Eid Tatu (Jumatano tarehe 28-06-2017) katika viwanja vya Soko la Kilombero stendi ya Hiace.
Sheikh Shariff Majini akiwasili kuendesha Dua maalum ya kuaga Mwezi mtukufu wa Ramadhani katika viwanja vya soko la Kilombero stendi ya Hiace jijini Arusha.
Sehemu ya umati wakati wa dua  hiyo katika viwanja vya soko la Kilombero stendi ya Hiace jijini Arusha.
 Sheikh Shariff Majini akiendesha Dua maalum ya kuaga Mwezi mtukufu wa Ramadhani. katika viwanja vya soko la Kilombero stendi ya Hiace jijini Arusha.
Sehemu ya umati wakati wa dua  hiyo katika viwanja vya soko la Kilombero stendi ya Hiace jijini Arusha.