Na Tulizo Kilaga, Mafinga

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Prof. Dos Santos Silayo amesema tatizo la uhaba wa mkaa jijini Dar es Salaam litakwisha kutokana na uwekezaji mkubwa uliofanywa na Kampuni ya Tractor inayomiliki kiwanda cha kuzalisha na kusambaza mkaa endelevu kilichopo Mafinga mkoani Iringa.

Kiwanda hicho kinatarajia kuanza uzalishaji mwishoni mwa mwezi huu kwa kuzalisha tani 40 za mkaa kwa siku na kuzisambaza katika jiji la Dar es Salaam, Mwanza na Dodoma kwa kuanzia kutokana na miji hiyo kuwa na matumizi makubwa ya mkaa hali inayohatatisha Misitu ya Asili nchini.

Akizungumza mara baada ya kujionea uwekezaji uliofanywa na kiwanda hicho, Prof. Santos alisema kuanzishwa kwa kiwanda hicho kinachozalisha na kusambaza mkaa inaouzalisha kutokana na takataka zitokanazo na uchakataji wa mbao na mabaki ya miti kwa teknolojia ya kisasa kutasaidia kupunguza matumizi makubwa ya mkaa katika miji mikubwa ambayo imekuwa kichocheo cha ukataji wa miti katika mikoa mingine.

Inakadiriwa kuwa karibu hekta 300,000 hadi 400,000 za misitu ya asili huharibiwa kila mwaka kutokana na utengenezaji mkaa.

Prof. Santos alisema kuanzishwa kwa kiwanda hicho kutasaidia kuongeza ufanisi wa matumizi ya mazao ya misitu ya kupanda, utapunguza utegemezi wa nishati ya kuni na mkaa kutoka misitu ya asili na kuongeza uhakika wa upatikanaji wa nishati ya mkaa kwa miji mikubwa nchini sambamba na kuongeza mchango wa sekta ya misitu kwenye ushiriki wa uchumi wa viwanda nchini Tanzania.

Hata hivyo alisema jitihada hizo zitafanikiwa ikiwa watumiaji wa nishati ya mkaa watabadilika na kuwa na mtizamo chanya juu ya matumizi ya mkaa mbadala pamoja na nishati nyingine mbadala.

“Tuongeze kasi katika kukabiliana na mabadiliko ya tabiawatu na kila mmoja kwa nafasi yake atimize wajibu wake ipasavyo, kwa pamoja tutafanikiwa kuinusuri nchi yetu kugeuka jangwa,” alisema.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa kiwanda hicho, Bw. Benjamin Lane alisema kiwanda hicho kitazalisha mkaa bora na kuhifadhiwa katika hali ya usafi kwenye mifuko ya kilo 50 na 25 kwa kuanzia ikiwa lengo nikuwa na mifuko hadi ya kilo moja itakayouzwa kwa bei rahisi zaidi ukilinganisha na bei ya mkaa halisi.

Lane alisema kuwa kiwanda hicho kimeamua kuwekeza kwenye uzalishaji mkubwa wa mkaa endelevu kwa lenga la kuiunga mkono serikali kutimiza adhima yake ya kuwa na matumizi endelevu ya misitu kwa faida ya vizasi vya sasa na vijavyo kwa kuhakikisha inatumia takataka zote zitokanazo na uchakataji wa mbao na mabaki ya miti kwa teknolojia ya kisasa kuzalisha mkaa.

Kwa upande wake, Meneja wa Shamba la Miti la Sao Hill, Bw. Saleh Baleko alisem shamba lake lina malighafi ya kutosha kukiwezesha kiwanda hicho kuwa na uzalishaji wa uhakika kutokana na wavunaji wengi nchini kutumia asilimia 70 tu ya eneo lote la uvunaji na kuacha asilimia 30 ikipotea ambayo sasa itatumika kuzalisha mkaa endelevu.

Akizungumza kuhusu mradi huo mmoja wa wananchi, Joyce Jonas alisema mradi huu ni mzuri na kuwaasa wawekezaji wengine kufanya uwekeza mkubwa kwenye mradi wa kuzalisha mkaa endelevu kutokana na kuwepo na mahitaji na matumizi makubwa ya mkaa ukilinganisha na viwanda vilivyopo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...