THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Tunaungana na Ulimwengu Kuokoa Bahari- Tizeba


Na Boss Brown

Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dkt. Chares Tizeba ataongoza ujumbe kutoka Tanzania kushiriki katika Kongamano la Bahari Duniani linalotarajiwa kuanza Jumatatu tarehe 5 hadi 9 katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa New York nchini Marekani.

“Changamoto inayoikabili bahari ni kubwa kutokana na uchafuzi utokanao na taka sugu ambazo zinahatarisha uhai wa Bahari yetu, tunaunagana katika kushilikiana na wadau mbalimbali katika juhudi za kuiokoa bahari kwa pamoja.” Alisisitiza Tizeba.

Akifafanua amesema kama nchi wanachama tanaadhimia kutekeleza kipengele cha 14 cha Malengo ya Maendeleo Endelevu 17 ya agenda ya 2030 ya Umoja wa Mataifa Kinacholenga matumizi bora ya rasilimali za baharini.

Kongamano hili ni la muhimu katika kuokoa bahari na litakutanisha Serikali, Umoja wa Mataifa, Mashirika yasiyo ya Kiserikali, Mashirika yanayoshughulikia mazingira, Taasisi za elimu na wanasayansi ya Jamii, Asasi za Kirai, watu binafsi, makampuni na viwanda.
Sehemu ya fukwe wa Bahari ya Hindi maeneo ya Jiji la Dar es Salaam ikiwa imeathiriwa na uchafu .