Katika kuhakikisha dhamira ya Serikali ya dhamira ya Serikali ya kujenga Uchumi wa Viwanda wadau wa kilimo na viwanda wamekutana ili kuzungumzia nafasi ya Benki ya Maendeleo ya Kilimo ya Tanzania (TADB) katika  kuhakikisha Benki hiyo inasaidia sekta ya Kilimo nchini.

Wakizungumza katika Kikao hicho kilichoandaliwa na TADB ili kujadili mikakati ya kuboresha uwezeshaji kwenye kilimo na viwanda nchini.
Akizungumza katika kikao hicho Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga amesema kuwa Benki imejipanga kuleta matokeo makubwa kwenye mapinduzi ya kilimo na viwanda hasa vya uchakakataji na usindikaji wa mazao ya kilimo.

Bw. Assenga amesema kuwa mipango hii itasaidia upatikanaji wa mali ghafi kwa viwanda vya ndani hivyo kusukuma ndoto ya Serikali kufikia lengo lake la Kujenga Uchumi wa Viwanda na kuhuisha uwekezaji kwenye Viwanda vidogo vidogo na vya kati vya usindikaji na uchakataji wa mazao ya Kilimo na mifugo.

“Benki imejikita kwenye kusaidia Sekta ya Kilimo iweze kusukuma dhamira ya Serikali ya Uchumi wa Viwanda uweze kutoa matunda yaliyokusudiwa ili kuchagiza na kusaidia Mapinduzi ya Kilimo kutoka kilimo cha kujikimu kwenda cha kibiashara ili kuchangia kwenye ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini,” alisema.

Bw. Assenga amesema katika kuhakikisha azma hiyo inatimia TADB imejipanga kutoa elimu ili kuwajengea uwezowakulima na taasisi mbali mbali za fedha pamoja na vyama vya ushirika kuweza kukopa toka TADB pamoja na kushirikiana na wadau mbali mbali kusaidia uwekezaji mkubwa kwenye Sekta ya Kilimo ili iweze kuinua pato la Taifa na kumkomboa Mwananchi.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji huyo ameongeza kuwa TADB imeanza kujiimarisha  na kuchochea mabenki na taasisisi za fedha kuongeza utoaji wa mikopo na fedha zingine kwenye Sekta ya Kilimo ili kuongoza utoaji mikopo ya uongezaji wa thamani katika shughuli za kilimo.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya Maendeleo ya Kilimo ya Tanzania (TADB), Bibi Rosebud Kurwijila (kushoto) akizungumza na aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mzee Peniel Lyimo (kulia) wakati wa Kikao cha Wadau wa Kilimo Kujadili Mikakati Ya Kuboresha Uwezeshaji Kwenye Kilimo Na Viwanda kinachofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC) Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Biashara ya TADB, Bibi Rehema Twalib (kulia) akizungumza wakati wa Kikao cha Wadau wa Kilimo Kujadili Mikakati Ya Kuboresha Uwezeshaji Kwenye Kilimo Na Viwanda kinachofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC) Dar es Salaam.
 Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mzee Peniel Lyimo (kulia) akiongoza Kikao hicho.
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga (kushoto) akisisitiza nafasi ya Benki yake katika kuleta matokeo makubwa kwenye mapinduzi ya kilimo na viwanda hasa vya uchakakataji na usindikaji wa mazao ya kilimo.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...