Na Munir Shemweta

Katibu Tawala MkoaTanga Bi. Zena Said amewataka wadau wa sheria kutumia fursa waliyonayo kuchangia kutoa maoni katika utafiti kuhusu taratibu zinazozuia haki jinai.Bi. Said alitoa rai hiyo wakati wa kufungua kikao cha wadau washeria mkoa wa Tanga juu ya utafiti kuhusu taratibu zinazozuia utoaji haki jinai kilichofanyika katika ofisi ya mkuu wa mkoa jijini Tanga.

Alisema, utoaji maoni yenye tija hususan kwa wadau wa mkoa wa Tanga siyotu utaisadia Tume ya KurekebishaSheria Tanzania katika mapitioya sharia hiyo bali kutaiwezesha nchi kuwa na mfumo wa sheria unaoendana na mabadilikoya jamii.

Kwa mujibu wa Katibu Tawala mkoa wa Tanga, mfumo wa utoaji haki jinai unakabiliwa na changamoto katika maeneo tofauti yanayohitaji kuangaliwa upya na kwa ukaribu ili kuhakikisha Tanzania inakuwa na sheria na taratibu zinazotoa haki kwa wananchi kwa wakati na haraka.

Awali Afisa Sheria Mkuu wa Tume ya Kurekebisha Sheria Bi. Anjela Shila, aliwaeleza washiriki wa kikao hicho ambao ni Mahakimu wa Mahakama za Mwanzo na Wilaya, maafisa Upelelezi wa polisi, Wanasheria wa Serikali, Mawakili wa Serikali na wa Kujitegemea , maafisa Magereza na Wanasheria kutoka Asasi za Kiraia zinazotetea haki za Jinai, Tume kwa sasa inaendesha utafiti kuhusu Mfumo wa Sheria ya Haki Jinai juu ya vipengele vinavyozuia haki.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Bi. Zena Said akifungua kikao cha Wadau wa sheria mkoa wa Tanga kutoa maoni juu ya utafiti kuhusu taratibu zinazozuia utoaji haki jinai kikao kilichofanyika ofisi za Mkuu wa mkoa jijini Tanga, kulia ni Afisa Sheria Mkuu wa Tume ya Kurekebisha Sheria Bi. Anjela Shila.
Katibu Tawala Mkoa wa Tanga akizungumza na Afisa Sheria Mkuu wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania Bi. Anjela Shila ofisini kwake kabla ya kufungua mkutano wa Wadau wa Sheria mkoa wa Tanga.
Mmoja wa wadau akiwasilisha maoni wakati wa Kikao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...