Wakazi wa Kijiji cha Ngulu kitongochi cha Mkongea wilaya ya Mwanga wamesema kuwa tatizo la maji limekuwa tatizo sugu kwa muda mrefu bila kutatuliwa hali inayosababisha ndoa nyingi kuvunjika. Mkazi wa kijiji hicho, Halima Miraji alisema kuwa tangu mwaka 2004 wamekuwa wakikabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa maji ambapo kwa muda mrefu sasa maji yamekuwa yakitoka usiku wa manane tu.

Halima alisema kuwa mfumo wa maji ulijengwa kwenye kijiji jirani cha Mgagani mwaka 1992 ambapo vijiji vyote viwili vilikuwa vikipata maji kutokea hapo. Hata hivyo, alisema wakati wa mafuriko, miundombinu iliharibika na hivyo kusababisha maji yapungue na ndipo viongozi wa vijiji hivyo viwili walipoamua kuwa maji yawe yanafunguliwa kwenye kijiji cha Ngulu nyakati ya mchana na kijiji cha Ngulu wakati wa usiku.

“Kutokana na changamoto hiyo, wanawake tunalazimika kuamka usiku wa manane kuchota maji kwa kuwa kwa kawaida huwa yanakatika alfajiri,” alisema Halima. Alisema kwa kuwa wanawake ndio wanaochota maji usiku na badhi ya wanaume wachache ambao hawajaoa, kutokana na hilo alisema kuwa badhi ya wanawake walijikuta wakiianza uhusiano na wanaume jambo ambalo limefanya ndoa zao kuvunjika.

Alisema kila mtu hulazimika kuweka ndo moja kwenye foleni ya maji iliyo na watu Zaidi ya hamsini kabla ya mzunguko kurudia mara ya pili, tatu na kadhalika jambo ambalo liliwafanya badhi ya wanawake kuingia kwenye vishawishi wakati wanasubiri kwenye foleni. Alisema kuwa changamoto nyingine, ni kuwa shughuli nyingi kama kilimo, biashara na kutunza familia zimekuwa zikizorota kwa kuwa wanakuwa wamechoka asubuhi baada ya kuchota bmaji usiku kucha.
Mkuu wa Wilaya yaMwanga, mkoani Kilimanjaro, Aaron Mbogho.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...