Mjumbe wa Serikali za Mtaa wa Mikocheni B, Kamati ya Mazingira Moses Sanga pamoja na Victoria Kileo wa Nipe Fagio wakiwa wamebeba taka wakati wa zoezi la kufanya usafi katika fukwe za Mbezi Beach leo Jijini Dar es Salaam. Zoezi hilo limeshirikisha Marafiki wa Bahari, Nipe Fagio,Mbezi Beach Neighborhoods. 
 Delicia Mwanyika and Cindy Tibazarwa kutoka Mbezi beach Neighborhoods wakishirikiana kuokota taka sugu kama vile Plastiki, makopo, nguo, viatu, nyavu, mataili, sindano, vyupa na taka nyinginezo.
 Beatrice Steyn Muasisi wa Mbezi Beach Neighborhoods akizungumza na waandishi wa habari wakati wa  zoezi la kufanya usafi wa fukwe ya Mbezi Beach katika kuokoa Bahari ambapo alisisitiza ushirikiano kutoka Serikali, Viwanda, Taasisi mbalimbali pamoja na watu binafsi kuungana kwa pamoja kurudisha uhai wa bahari ambayo inaelekea kufa kama hakuna hatua itakayo chukuliwa sasa.
 Boss Brown Muasisi wa Marafiki wa Bahari kutoka Mikocheni B akiwa katika zoezi la kufanya usafi katika fukwe za Mbezi Beach leo Jijini Dar es Salaam. Zoezi hilo limeshirikisha Marafiki wa Bahari, Nipe Fagio,Mbezi Beach Neighborhoods
Washiriki wa zoezi la usafi wa fukwe wa Mbezi Beach wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumaliza kwa zoezi hilo leo Jijini Dar es Salaam. Zoezi hilo ni harakati za kuunga mkono kampeni ya kuiokoa Bahari ambalo limeshirikisha asasi za Nipe Fagio, Mbezi Beach na Friends Of Ocean kutoka Mikocheni B chini ya udhamini wa Nabaki Africa, Koncept Communication Pamoja na AFM 92.9 ya mjini Dodoma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...