Na Zainab Nyamka, Globu ya Jmaii.

Eneo la Barabara  ya Mtoni Kijichi yenye urefu wa Kilo
mita 0.9 ikiwa imeharibiwa na mvua na kusababisha kufungwa kwa barabara hiyo kwa muda wa mwezi mmoja sasa.

Barabara hiyo ni njia kuu ya wapita kwa miguu na magari  pia kutokana na njia hiyo kuunganisha maeneo ya Kota za Benki, Nasako, Kota za Polisi na Jeshi  na Polisi na shule ya Sekondari Neluka na Shule ya Sekondariu ya Mbagala Kuu.

Wananchi wa eneo hilo wamesema kuwa barabara hiyo inahatarisha sana kwani watoto wao wamapokuwa wanapita katika  njia hiyo wanaweza wakajisahau na kutaka kuchungulia ili kuona ndani kuna nini na kuweza kuanguka pia, pia kuna baadhi ya watoto ambao ni watundu huamua kuingia ndani ya shimo na wengine kushindwa kutoka.

Wameiomba serikali kuikarabati barabara hiyo ambayo inaunganisha maeneo makubwa ya kata ya Kijichi.
 Picha mbalimbali zikionesha jinsi barabara ya Mtoni Kijichi inayounganisha maeneo ya Kata ya Kijichi na kusababisha baadhi ya mahitaji muhimu kukosekana kwa takribani mwezi mmoja.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...