Mabingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara Yanga imekuwa timu ya kwanza toka Tanzania kutinga nusu fainali ya Sports Pesa Super Cup kwa mikwaju ya penati. 
Katika mchezo wa kwanza Singida United ilicheza dhidi ya AFC Leorpads ya Kenya na vijana hao wa Hans Van Der Pluijm walitolewa  kwa  penalti 5-4 
Yanga imeing’oa Tusker ya Kenya kwa mikwaju ya penalti 4-2 baada ya dakika 90 kukamilika kwa sare ya bila bao. 
 Kipa wa Yanga, Deo Munishi maarufu kama Dida alichangia kung’olewa kwa Tusker baada ya kupangua moja ya mikwaju ya Wakenya hao. 
Yanga sasa watakutana na AFC Leorpads siku ya Alhamis na Fainali ya Michuano hiyo itachezwa siku ya Jumapili Juni 11 na bingwa atacheza na Everton katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam July 13 mwaka huu.
 Mshambuliaji wa Yanga Chipukizi, Said Mussa, akijipinda kupiga shuti katikati ya mabeki wa Tusker, wakati wa mchezo wa mashindano ya SportPesa Super Cup, katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam. 
 Mshambuliaji wa Yanga Chipukizi, Said Mussa, akimtoka beki wa Tusker, Corins SHivachi, wakati wa mchezo wa mashindano ya SportPesa Super Cup, katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam. 
 Juma Mahadhi wa Yanga (kushoto) akichuana na beki wa Tusker, James Situma, wakati wa mchezo wa mashindano ya SportPesa Super Cup, katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
 Yanga Chipukizi na Tusker ya Kenya wakichuana katika mchezo wa mashindano ya SportPesa Super Cup, katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam. Picha zote na Montage Ltd

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...