THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

BASHE AWEZESHA VIKUNDI VYA WAJASIRIAMALI NZEGA MJINI

Katika Sherehe za Mwenge wa Uhuru zilizofanyika katika Uwanja wa Parking wilayani Nzega mkoani Tabora; Mbunge wa Jimbo la Nzega Mjini Mhe. Hussein Mohammed Bashe amekabidhi hundi ya Shilingi za Kitanzania Milioni Tatu na Laki Tisa (Tzs 3,900,000) kwa ajili ya kuwezesha vikundi mbalimbali vya wajasiriamali vilivyojitokeza kwenye sherehe hizo kuweza kumudu gharama za uendeshaji wa ofisi zao.
Hundi hiyo ilikabidhiwa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge kitaifa Bw. Amour Hamad Amour ambaye hakusita kusifia juhudi za Mheshimiwa mbunge kila mahali alipotembelea miradi ya maendeleo na huduma za jamii iliyokuwa anatekelezwa na Mhe. Hussein Bashe jimboni kwake na ndani ya Halmashauri ya Mji wa Nzega.
Bw. Amour H. Amour anasema.... "Tumetembea maeneo mengi, majimboni na wilayani, tumezunguka tukiukimbiza Mwenge kila mahali; wabunge wamejitokeza kushiriki zoezi hili lakini Mhe. Bashe amekua nasi bega kwa bega na ushirikiano wake umekua ni mkubwa sana. Haitoshi mambo anayoyafanya kwa wananchi wake ni mambo makubwa, ya kuigwa na kuungwa mkono"
Kwa upande waje Mkuu wa Wilaya ya Nzega Mhe. Godfrey Ngupula alisema...."Kiongozi wa mbio za Mwenge, kuna msemo usemao msifie mtu angali yupo hai; nami leo nasema Mhe. Bashe anafanya kazi kubwa sana. Hapa tulipo tayari Mhe. Bashe amewapa ufadhili na amewalipia ada wanafunzi wote waliofaulu kujiunga na kidato cha Tano kwenye shule mbalimbali za serikali nchini, haitoshi bado anapambana kuhakikisha elimu ndani ya Jimbo la Nzega Mjini inakua na ufaulu unaongezeka"
 Kiongozi wa Mbio za Mwenge kitaifa Bw. Amour Hamad Amour akikabidhi  mfano wa hundi ya Shilingi za Kitanzania Milioni Tatu na Laki Tisa (Tzs 3,900,000) kwa ajili ya kuwezesha vikundi mbalimbali vya wajasiriamali.