Na Karama Kenyunko Globu ya jamii.

TAASISI ya Elimu, British Council  inawaalika watanzania wote wanaopenda kujifunza kiingereza kujitokeza kwa wingi kwenye banda lao la sabasaba kwa ajili ya kufanya mtihani na kupunguza garama.

Taasisi hiyo inatumia maonesho ya 41 ya kimataifa ya Biashara  ya  Dar e Salaam (DITF) kutoa mitihani ya kiwango cha lugha ya Kiingereza bure kwa wananchi  wanaohitaji,lengo likiwa ni kujipima ufahamu wao. Meneja wa Maendeleo na Biashara kutoka British Council, Amata Bosco amesema hayo leo katika maonyesho yanayofanyika katika barabara ya Kilwa.
 Mkurugenz wa British Council Nchini, Angela Hennely akizungumza na waandish was habari katika mkutano huo.

Amesema kwa Tanzania kuna uhitaji  mkubwa wa kukuza lugha ambapo watu wengi wamejitokeza katika banda hilo kwa ajili ya kufanya mitihani hiyo yenye kujipima kiwango chao cha Kingereza. 
Amesema  mtihani wa kiwango unaofanyika katika maonesho hayo ni bure unapunguza garama kubwa wa watu wanaopenda kujifunza kiingereza kwa kuwa ukifanyia mtihani huo shuleni kwao unalazimika kulipia sh.48,000.

"kufanyika kwa mitihani hii ya kiwango katika maonesho kutasaidia watanzania walio wengi kuokoa kiwango cha fedha ambacho hukitumia wakati wa kawaida kwa kwenda kusoma katika taasis hiyo", amesema.
"Lengo kubwa la kufanya mtihani huu bure ni  kuhamasiha watu kujiandikisha kwa wingi katika kozi mbalimbali zitolewazo na taasisi hiyo ili kuboresha lugha ya Kiingereza.  Aidha amesema Taaasisi hiyo inawaunganisha watu na Uingereza katika ubunifu na vitu mbalimbali napia kujifunza masuala mbalimbali kutoka nchi hiyo. 

Amata amewaasa, watanzania  wanaopenda kujifunza ama kufundisha  Kiingereza kujitokeza kwa wingi, kufanya mitihani,  katik taasisi hiyo kwani ni  eneo muhimu la kuanzia na kwamba ndio maana wanatumia maonesho hayo maarufu kama sabasaba kwa ajili kuweza kuwafikia walio wengi Zaidi. 

" Mtihani huu wa kiwango wa  Kiingereza unafanyika kila siku ya maonesho na watu wengi wamekuwa wakifika hapa wakiwepo wenye kiwango cha chini, cha katikati na hata kiwango cha juu lakini pia wapo wasiojiamini katika kuzungumza lugha hiyo ambao na wamekuwa wakifika. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...