Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Mhe. Juma Zuberi Homera ametoa msaada wa bati 100 na mifuko ya saruji 100 kwa shule ya msingi msinjili iliyopo kijiji cha msinjili kata ya Mlingoti magharibi Tarafa ya Mlingoti.
Dc Homera ameainisha matumizi ya msaada huo kama ifuatavyo, bati 25 na mifuko 50 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa madarasa mawili ya shule ya msingi msinjili Iliyopo katika kijiji cha msinjili na Bati 60 pamoja na mifuko 50 ya saruji kwa ajili ya kuezeka nyumba za walimu wawili wa shule ya msingi mwangaza zilizoezekwa kwa nyasi, sambamba na hayo aliagiza madarasa katika shule hio zikarabatiwe.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...