MKUU wa Wilaya  ya  Kibaha Mhe. Asumpta Mshama  (pichani)  ametoa onyo  kali kwa  wamiliki wote wa ardhi ambao wanazimiliki kwa muda mrefu bila kuziendeleza hali inayopelekea kuzalisha mapori yanayoficha vitendo vya  kihalifu Kibaha Mkoani Pwani.
Bi Mshama amesema hayo leo akiwa katika  mkutano wa hadhara uliofanyika maeneo ya Visiga , Kibaha Mkoani Pwani ambapo aliweza kupokea changamoto mbalimbali kutoka kwa wananchi wa eneo hilo  ikiwa ni pamoja na tishio la kuzungukwa na mapori yenye wanyama wakali pamoja na kuwa  maeneo ya yanayofanyika vitendo viovu.


"Wamiliki wote wenye maeneo makubwa  ya  ardhi  ambazo haziendelezwi serikali itawapokonya ifikapo Septemba Mosi mwaka huu" amesema Mhe. Mshama.

Akiwa kwenye muendelezo wa ziara yake Wilaya ya Kibaha  alisema  wamiliki wenye maeneo makubwa wamekuwa wakizalisha  mapori ambayo yamekuwa  vichaka vya kufanyia vitendo viovu ndani ya Mkoa wa Pwani huku akitolea mifano ya mapori yaliyopo Wilaya ya Kibiti.
Ameongeza kwa kusema kuwa yuko tayari kwenda Mahakamani kwa kuwang'anya ardhi wamiliki wasioendelwza maeneo hayo huku akisema kuwa hati zimeandikwa mwisho wa kuendeleza eneo ni miaka mitatu huku akiongeza kwa kusema kuwa  baada ya kuzichukua ardhi hizo fomu zitatolewa kwa wananchi ili wazijaze nankugaiwa maeneo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...