Waziri wa Habari, Utamaduni, Michezo, Sanaa na Burudani, Dkt. Harrison Mwakyembe amewashukuru Watanzania kwa ushirikiano mkubwa waliompa katika kuombeleza kifo cha mkewe Linah Mwakyembe kilichotokea usiku wa Julai 15 mwaka huu kwenye Hospitali ya Aga Khan ya Jijini Dar es salaam.
Dkt. Mwakyembe pia amemshukuru Rais John Magufuli, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwa mchango mkubwa walioutoa katika kumuuguza mkewe.
Dkt. Mwakyembe ametoa shukrani hizo  Julai 26 wakati akizungumza na wanahabari nyumbani kwake Kunduchi wilayani Kinondoni.
Mbali na hao, Dkt. Mwakyembe ambaye pia ni Mbunge wa Kyela Mkoani Mbeya, amewashukuru viongozi wote wa dini akiwamo Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Aboubakar Zuberi na maaskofu.
"Wanafamilia tutakumbuka moyo adhimu na upendo na ushirikiano tulioupata kutoka Katibu Mkuu wa wizara hii Profesa Elisante Ole Gabriel na viongozi wengine waandamizi wa Serikali. Mwisho kabisa Wanakyela kwa uvumilivu wao katika kipindi hiki kigumu," amesema Dkt. Mwakyembe.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza na waandishi wa habari (hawapo katika picha) leo Jijini Dar es Salaam alipokuwa akitoa neno la shukrani kwa wote walioshiriki katika kumfariji kipindi cha msiba wa mke wake mpendwa Bi. Linah George Mwakyembe.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...