Duka la kadi mbalilmbali za mialiko ya sherehe limezinduliwa Mwenge,jana jijini Dar, ambapo kila mtu anaweza kumudu gharama.

Akizungumza baada ya kufunguliwa duka hilo Mkurugenzi Mtendaji wa R Plus , Rehema Moses amesema kuwa wameweka kadi zinazoendana na wakati katika sherehe na hafla  mbalimbali.

Amesema Kadi za mialiko walizo nazo ni Send off ,KitchenParty , Harusi pamoja na mialiko ya Kiofisi zinazokwenda kisasa na wakati zaidi.

Rehema amesema katika biashara hiyo wajasirimali wengine wanaweza kununua hapo kwa bei ya jumla kutokana na mahitaji yao.

Amesema kadi zinazopatikana  za aina zote za kumfanya kila mtu kuweza kumudu kwa gharama nafuu kutokana na uwezo wake.
Mgeni Maalum wa Ufunguzi wa Duka la Kadi Mwenge, Doris Mollel Foundation, Doris Mollel akikata utepe kuashiria uzinduzi wa duka la kadi Mwenge.
Mkurugenzi Mtendaji R Plus na Mmiliki wa Duka la Kadi za Mialiko, Rehema Moses akimuonesha kadi mbalimba mgeni maalum wa ufunguzi wa Duka, Doris Mollel katika hafla iliyofanyika Mwenge.
Mkurugenzi Mtendaji R Plus na Mmiliki wa Duka la Kadi za Mialiko, Rehema Moses akiwa na Mwenza wake wakikata keki mara baada ya duka hilo kufunguliwa.
Mgeni Maalum, Doris Mollel akiwa na Mmiliki wa Duka, Rehema Moses na wadau mbalimbali waliofika katika duka hilo wakibadilishana mawazo mara baada ya uzinduzi
Picha ya Pamoja.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Nahitaji huduma ya kadi na nipo mbali nitapaje

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...