Emirates
imewapa baadhi ya familia za kitanzania ladha ya ushindi wa usafiri wa
anga wakati walipohudumia kundi la wazazi na watoto wao katika moja ya
sinema kali ya Despicable Me 3.
Sinema
mpya iliyotoka katika anga ya dunia- karibia watoto 30 na wazazi wao na
walezi walihudhuria uzinduzi huo uliofanyika Mlimani City Mall IMAX
tarehe 8 Julai 2017 kuangalia sinema bora uliyovuta hisia za wengi
ikifatiwa na chakula cha mchana sehemu hiyo hiyo iliyoandaliwa na
mwenyeji mkurugenzi wa Emirates Tanzania, Rashed Alfajeer.
Emirates
pia ilipata uzoefu wa familia katika kutangaza ofa ya 50% katika daraja
la uchumi kati ya abiria 2 - 8 kusafiri wote katika sehemu 21
zilizopendekezwa kama Uarabuni, Ulaya vile vile Marekani kusini na
kaskazini. Hiyo ofa ni kati ya tarehe 6 na 14 julai 2017 na za nje kati
ya tarehe 6 julai na 10 Disemba 2017.
Rashed Alfajeer, Mkurugenzi Mkuu wa Emirates Tanzania alisema: " Emirates ipo kwa ajili ya kutoa thamani kwa pesa na wamejihakikisha kutoa huduma iliyo bora angani mpaka ardhini na hakuna tofauti linapokuja swala la familia katika kusafiri. Kwa watoto, lazima wawekwe huru na waburudike na kuwajali kwa kuwapa wigo mpana katika kuchagua sinema na programu ili kukithi mahitaji yao".
Ofa hii maalum inatoa nafasi kubwa kwa familia kuwa na likizo ya pamoja sehemu mbali mbali kwa gharama nafuu kwa muda uliowekwa tu na kuongeza wakati wakisafiria na Emirates, familia itarajie kupata wigo mpana wa program za watoto ikiwa na channeli 90 mahususi kwa ajili ya kuwaburudisha watoto ikiwamo pamoja na sinema bora na programu za TV kutoka Disney, Cartoon Network, Cbeebies Na Nickelodon na nyingine nyingi.
Chakula
pia upewa kipaumbele sana pindi abiria wawapo angani kwenye Emirates.
Watoto wenye umri kati ya miaka 2 na 12 hupewa chakula maalum
wakihudumiwa katika vyombo vya kisasa wakiwa na staff pamoja na
marubani. Wasafiri wenye ugunduzi wachache wanaweza kupata marafiki
wapya pindi wawapo safarini, kuna blanketi kwa ajili ya kujifunika na
kuweza kujiburudisha na majarida yanayokuja Dar Es Salaam kila siku.
Ndege ya EK 0725 inatoka Dubai saa 10:25 na kufika Dar Es Salaam saa
14:50. Ndege inayorudi EK 0726 inatoka Dar Es Salaam saa 16:45 na kufika
Dubai saa 23:20.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...