MKAZI wa Kigamboni, jijini Dar es Salaam leo amefanikiwa kuibuka na ushindi mnono wa Sh Milioni 20 baada ya kutangazwa mshindi katika kinyang’anyiro cha droo ya 23 ya Bahati Nasibu ya Biko ‘Ijue Nguvu ya Buku’, inayoendelea kutesa hapa nchini.

Droo iliyompa ushindi mnono mkazi huyo wa Kigamboni maarufu kama ‘Jumadili’, imechezeshwa jijini Dar es Salaam na Balozi wa Biko Kajala Masanja akishirikiana na mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Bakari Maggid.

Akizungumza katika droo hiyo ya aina yake, Meneja Masoko wa Biko Tanzania, Goodhope Heaven, alisema kumpata mshindi wao wa Kigamboni ni sehemu ya kuhakikisha kuwa washindi wao wanaendelea kuzoa mamilioni kutoka kwao baada ya kucheza Biko.

Alisema kila anayecheza Biko anasehemu kubwa ya kuibuka na ushindi wa zawadi za papo kwa hapo pamoja kuanzia Sh 5,000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni moja bila kusahau donge nono la Sh Milioni 20 linalotoka katika droo kubwa za Jumatano na Jumapili.

“Kucheza Biko ni rahisi kwa sababu mchezo wetu wa kubahatisha unachezwa kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi kwa kupitia miamala ya kifedha kuanzia Sh 1,000 na kuendelea ambapo namba zetu za kampuni ni 505050 na ile ya kumbukumbu ni 2456.

“Ili mtu aweze kushinda anapaswa kucheza mara nyingi zaidi kwa kuanzia Sh 1000 na kuendelea ambapo mbali na ushindi wa papo kwa hapo unaotoka kila wakati, pia ni fursa nzuri ya droo kubwa ya Sh Milioni 20 ambazo tunaamini mtu akifanikiwa kuzipata kama alivyopata mshindi wetu wa Kigamboni bwana Nyari maisha yake yatapiga hatua kubwa,” Alisema. 
Mwakilishyi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Bakari Maggid kushoto akiandika dondoo muhimu katika droo ya 23 ya Bahati Nasibu ya Biko 'Ijue Nguvu ya Buku' leo jijini Dar es Salaam, ambapo mkazi wa Temeke, Fredy Nyari alifanikiwa kuibuka na ushindi mnono wa Sh Milioni 20 kutoka Biko. Kulia ni Balozi wa Biko Tanzania, Kajala Masanja.
Harakati za kumtafuta mshindi wa droo ya 23 Fredy Nyari wa Kigamboni jijini Dar es Salaam, zilipofikia ukomo kwa Balozi wa Biko, Kajala Masanja kutoa neno kwa wadau na Watanzania kwa ujumla juu ya bahati nasibu ya Biko.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...