THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

ILALOO FC MABINGWA KOMBE LA DIWANI SARANDA

MASHINDANO ya ligi ya kombe la Diwani wa kata Saranda, Tarafa ya Kilimatinde, wilayani Manyoni, Mkoani Singida yamefikia tamati kwa timu ya soka ya ILALOO FC kuwa mabingwa wa kombe hilo kwa mwaka huu wa 2017 baada ya kuifunga timu ya Saranda FC kwa jumla ya magoli 2-1.

Ligi hiyo iliyoanza kuchezwa juni, 29 mwaka huu kwa makundi mawili yaliyokuwa yakivitumia viwanja vya michezo vya Shirika la reli Tanzania (TRC) ilizishirikisha jumla ya timu sita za kata hiyo ambazo ni pamoja na Saranda FC, Ilaloo FC, Irucha, Mlimani A, Mlimani B na Mhegahega FC.

Akitangaza matokeo ya mashindano hayo, Katibu wa Chama Cha mpira wa miguu wilaya ya Manyoni (MADIFA), Joshua Msemakweli aliwataka vijana hao kuwekeza kwenye mchezo wa soka kwa kuamini kwamba michezo ni afya na michezo ni ajira.  

“Mashindano ngazi ta kata ya Saranda yalishirikisha timu sita kutoka katika vijiji na vitongoji,ambavyo ni Kijiji cha Saranda ambapo ndipo makao makuu ya kata  pia Ilaloo na Irucha zipo Kijiji cha Saranda Kijiji cha Saranda kilikuwa na timu tatu”alifafanua Msemakweli.

Kwa upande wake muandaaji wa kombe hilo ambaye pia ni diwani wa kata ya Saranda,Joseph Ndahani aliyataja baadhi ya malengo ya michezo hiyo kuwa ni kuhakikisha wanakuza pamoja na kuvitangaza vipaji wa vijana wa kata hiyo kupitia sekta ya michezo.

Naye Mwalimu wa timu ya soka ya Ilaloo FC ambao ndiyo mabingwa wa kombe hilo, Rashid Juma alikishukuru kituo hiki kwa kuweza kufika katika Kata hiyo na kuwawezesha kusikika maana haijawahi kutokea bahati kama hiyo kwa vituo vingine kufika huko. 
Katibu wa Chama Cha Mpira wa miguu wilaya ya Manyoni (MADIFA) Joshua Msemakweli (wa pili kushoto) akitoa maelekezo kwa viongozi wa timu pamoja na wachezaji wa timu zilizoshiriki mchezo wa fainali katika kata ya Sanjaranda.