Na Jumia Travel Tanzania
Jumia kwa mara ya pili mfululizo imeorodheshwa na Taasisi ya Kiteknolojia ya Massachusetts (MIT) ya nchini Marekani kuwa ni miongoni mwa makampuni 50 bora yanayotumia teknolojia katika biashara ili kurahisisha utoaji na upatikanaji wa huduma.
Kwenye orodha hiyo ambayo hujumuishwa makampuni makubwa ya kiteknolojia duniani kama vile Apple, Amazon, Facebook na Alibaba, Jumia kwa mwaka huu wa 2017 imetajwa kushika nafasi ya 44 kutokea nafasi ya 47 iliyoishika mwaka 2016.
MIT imeiatambua Jumia ambayo ilianzishwa mwaka 2012 ikijulikana kama Africa Internet Group (AIG) kwamba ni miongoni mwa makampuni ya awali kuchipukia barani Afrika, ikiwa na thamani ya dola za Kimarekani bilioni moja kutoka dola za Kimarekani milioni 327 ambapo ilimjuisha Goldman Sachs kama mmojawapo wa wawekezaji wake.
Ikiwa inajishughulisha na utoaji wa huduma mtandaoni kwenye maeneo kama vile manunuzi ya bidhaa, usafiri, chakula, makazi na magari ambazo zote zinatumia jina la Jumia, kampuni hiyo inapambana na changamoto za kufanya biashara kwa njia ya mtandao barani Afrika zikiwemo barabara zisizopitika kwa urahisi, wateja wasiotabirika, kukosekana kwa mtandao wa intaneti kwenye baadhi ya maeneo ambapo lengo kubwa ni kuwashawishi watu wa tabaka la kati kufanya matumizi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...