KAMPUNI ya kimataifa inayojihusisha na utengenezaji na uuzaji wa vifaa vya mbalimbali vya mapishi kwenye hoteli , PiMAK imefungua duka hapa nchini lililopo Mnazi Mmoja, Dar es Salaam.

Meneja Mkuu wa kampuni hiyo, Ali Donmez alisema, kampuni hiyo imebainisha soko kubwa la bidhaa zake hapa ambapo imekuwa ikifanya biashara kwa muda mrefu kwa kushirikiana na mawakala, na kwa sasa licha ya kufungua duka hilo lakini bado inaona kuna fursa kubwa zaidi za uwekezaji.

Akizungumzia kuhusiana na bidhaa hizo, alisema kuwa ni bidhaa kwa ajili ya matumizi ya hoteli, migahawa na huduma kubwa za mapishi vikiwamo vya kukatia nyama, kuhokea mikate, kuoshea vyombo, kupikia na huduma nyingine za kihoteli. 

Aliongeza kampuni hiyo imeshafanya kazi hapa nchini kwa miaka minne ikishirikiana na mawakala ambapo vifaa hivyo vinatumiwa na hoteli nyingi hapa nchini, huku akiweka wazi kuwa inatoa huduma za utengenezaji wa bidhaa hizo pia. 

"Kampuni hii ina miaka 25 na makao yake makuu ni Instabul, Uturuki kwa Tanzania tumekuwapo kwa miaka minne tukifanya biashara kwa kushirikiana na mawakala lakini leo tumefungua (jana) tumefungau duka letu huku tukiwa na lengo na kuja kuanzisha kiwanda cha uundwaji wa vifaa hivi hapa hapa nchini" alisema Donmez. 

Pia alisema kuwa kampuni hiyo kwa miaka ya baadae itafungua kiwanda hapa nchini kwa lengo la kurahisha upatikanaji wa bidhaa zake kwenye soko la Afrika Mashariki na Kati na pia kuongeza ajira zaidi kwa watanzania.
Kampuni hiyo kwa sasa inafanya kazi nchi 16 na kwa hapa nchini imeshaajiria wafanyakazi 15 huku ikitoa huduma za ukarabati wa vifaa vya upishi hoteli mbalimbali nchini.
 
Mmiliki wa Kampuni ya PiMAK, Riza Ergun akikata utepe kuashiria uzinduzi wa duka la kuuza vifaa mbalimbali vya mapishi lililofunguliwa eneo la Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. 
Mmiliki wa Kampuni ya PiMAK, Riza Ergun akiwa na wadau kadhaa waliojitokeza kwenye uzinduzi huo wakisoma menu ya baadhi ya vifaa vinavyouzwa dukani hapo mara baada ya kuzinduliwa
Wafanyakazi na wageni waliojitokeza siku hiyo ya uzinduzi wa duka la kuuza vifaa mbalimbali vya mapishi wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kufunguliwa eneo la Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...