Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, ameutaka uongozi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), kuweka mikakati endelevu ili kuwezesha kiwanja cha ndege cha Tabora kujisimamia na kujiendesha kutokana na miundombinu bora na ya kisasa inayoendelea kujengwa kiwanjani hapo.

Amezungumza hayo jana mkoani humo, mara baada ya kuanza ziara ya kikazi ambapo pamoja na mambo mengine Waziri Prof. Mbarawa amekagua na kujionea maendeleo ya mradi wa ujenzi wa kiwanja hicho ambapo mpaka sasa ujenzi wake umefikia asilimia 96 na umegharimu kiasi cha shilingi Bilioni 27.

“Hivi sasa huduma ya usafiri wa ndege katika kiwanja hichi unaridhisha, hivyo ongezeni ubunifu ili kuvutia abiria wengi na kuwezesha kiwanja kujiendesha”, amesema Prof. Mbarawa.

Amesisitiza kuwa gharama za usafiri wa anga zitaendelea kupungua kadri huduma na ubora zitavyokuwa zinaendelea kuongezeka ili kuwezesha abiria wengi zaidi kutumia usafiri huo na hivyo kuwezesha pato la Taifa kuongezeka.
Meneja wa Mradi wa ujenzi wa kiwanja cha ndege cha Tabora Eng. Neema Joseph, akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, kuhusu maendeleo ya ujenzi yaliyofikiwa kiwanjani hapo, wakati akikagua ujenzi wake, mkoani humo jana.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, akitoa maelekezo kwa Meneja wa Mradi wa ujenzi wa kiwanja cha ndege cha Tabora Eng. Neema Joseph, wakati akikagua maendeleo ya ujenzi ya kiwanja hicho uwanjani hapo, jana.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kulia), akitoa maelekezo kwa Mkandarasi wa Kampuni ya Kaya-Ceytun JV Eng. Ifran Sakrak (kushoto), wakati alipokuwa akikagua maendeleo ya ujenzi ya kiwanja cha ndege cha Tabora, jana.
Muonekano wa Taa za kuongozea ndege wakati wa kutua zilizojengewa katika Kiwanja cha Ndege cha Tabora.
Muonekano wa Mtambo wa kisasa wa kuongoza ndege unaonesha mwelekeo na umbali wa zaidi ya Kilomita 200 uliopo katika kiwanja cha ndege cha Tabora.

SOMA ZAIDI HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...