Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Magonjwa yasiyoambukizwa yanaweza  kuepukika kwa kutumia vyakula vya asili pamoja na kufanya mazoezi ambapo hakuna gharama inaweza kufanya mtu kuchangia. Magonjwa hayo ambayo ni Kisukari, shinikizo la Damu, pamoja na Unene wa kupindukia.

 Hayo aliyasema Mwenyekiti wa Kikundi cha Mtambani  kilichopo Mlandizi wilayani Kibaha, mkoani Pwani, Mohamed Pongwe wakati akizungumza na Michuzi Blog, amesema kuwa magonjwa yasiyombukizwa yanaweza kuepukika kwa kula vyakula visivyo na mafuta pamoja na kufanya mazoezi katika mazingira wanayoishi.

Amesema walipata elimu baada ya Shirika la Help Age International  kupitia mradi wa Afya kwa Rika Zote  ambapo  waliweza kuanza ufugaji wa kuku pamoja na kilimo cha mboga mboga.

Pongwe amesema kuwa wanafanya kilimo cha mboga mboga  na ufugaji wa kuku  ambapo wanauza na fedha zinazopatika zinaingia katika kikundi pamoja na wao wenyewe kula mboga mboga na mayai na nyama za kuku hali ambayo imeweza kuboresha afya zao.

Aidha amesema katika miradi hiyo wameza kupata laki tano ambapo uzalishaji unaendelea katika maeneo yote ikiwa ni pamoja na kubadilika kiuchumi katika kikundi.
 Mwenyekiti wa Kikundi Cha Mtambani, Mohaamed Pongwe akizungumza  katika sehemu wanayofanya kilimo cha mboga mboga.
 Mwanakikundi, Mwajuma Fanuel akizungumza na katika sehemu ya kilimo cha mbogamboga .
 Baadhi ya wanakikundi wakiweka mbolea ya kinyesi cha kuku katika shamba la mbogamboga.
Wanakikundi wa Mtambani Mlandizi wakiwa katika picha ya pamoja 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...