Pichani ni Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, Albert Msole (CCM) ambaye amefanikiwa kushinda tena nafasi hiyo baada ya kumbwaga mpinzani wake Philemon Oyogo (Chadema).    
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya hiyo, Yefred Myenzi akitoa matokeo hayo alisema kati ya madiwani 22 waliopiga kura, madiwani 14 walimpigia Msole na madiwani nane walimpigia Oyogo. 
Myenzi alisema Msole atadumu kwenye nafasi hiyo kwa kipindi cha mwaka mmoja wa 2017/2018 ndipo utakapofanyika uchaguzi mwingine wa makamu Mwenyekiti. Akizungumza baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa nafasi hiyo Msole aliwashukuru madiwani wote kwa heshima kubwa waliyompa na kumrudishia tena nafasi hiyo hivyo ataendelea kushirikiana nao kuhakikisha kuwa halmashauri hiyo inasonga mbele kwenye maendeleo. 

"Tuendelee kushirikiana pamoja kwani tumeshirikiana vizuri tangu mwaka 2015 na kazi yangu kubwa ni kumsaidia Mwenyekiti wa halmashauri yetu, natoa ahadi kwenu kuwa nitaendelea kuteleleza wajibu wangu kwani heshima mliyonipa ni kubwa japo mimi ni mdogo kwenu," alisema Msole.  
Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Jackson Sipitieck alisema kama siyo jambo la kisheria, kanuni na taratibu, wasingeruhusu uchaguzi huo ufanyike kwani jitihada za Msole za uchapakazi kwenye halmashauri hiyo zinajulikana. 
"Msole ni mpambanaji mzuri, muwajibikaji, muwazi na anayefanya kazi zake kwa kutenda haki bila kupendelea mtu na nadhani wote tunatambua jitihada zake kama siyo sheria angekuwa makamu Mwenyekiti kwa miaka yote mitano," alisema Sipitieck.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...