Mkutano wa 29 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU) amefunguliwa rasmi Jijini Addis Ababa- Ethiopia ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli anawakilishwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan katika mkutano huo 

Mkutano huo wa Wakuu wa Nchi na Serikali unaofanyika katika Makao Makuu ya Umoja wa Afrika Jijini Addis Ababa- Ethiopia na utajikita katika kujadili masuala mbalimbali yanayohusu umoja huo ikiwemo hali ya ulinzi na usalama katika Bara la Afrika hasa kwenye nchi za Sudan Kusini, Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo- DRC na Libya.

Aidha, Viongozi hao watajadili hali ya usalama kwenye baadhi ya nchi ambazo ziliathiriwa na kundi la Boko Haram za Nigeria, Niger, Chad na Cameroon.

Wakuu hao wa Nchi na Serikali wa AU pia watajadili kwa kina kuhusu uanzishwaji wa eneo huru la kibiashara katika bara la Afrika kwa ajili ya kuliendeleza Bara hilo kwa ajili ya kukuza biashara baina ya nchi wanachama, uwekezaji, kuondoa vikwazo vya kibiashara pamoja na kupunguza utegemezi kwa masoko ya nje.

Mambo mengine yatakayojadiliwa na Viongozi hao ni bajeti ya Umoja huo, mpango mkuu kuhusu hatua za kivitendo za kuzuia mapigano katika Afrika kufikia mwaka 2020, maboresho katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na maboresho ya kitaasisi katika AU.

Kwa upande wa Tanzania, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan anaongoza ujumbe wa Tanzania katika mkutano huo ambao unahudhuriwa pia na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt Augustine Mahiga na Waziri wa Kazi,Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Maudline Cyrus Castico pamoja na Watendaji wengine wa Serikali. Kauli Mbiu ya Mkutano wa mwaka huu ni Kuimarisha Mgawanyiko wa Idadi ya Watu Kupitia Uwekezaji katika Vijana. (Harnessing Demographic Divident Through Investments in the Youth)
Picha ya pamoja 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amemwakilisha Rais wa John Pombe Magufuli katika mkutano wa AU katika Makao makuu ya Umoja huo Addis Ababa- Ethiopia.Mkutano umefunguliwa hii Leo Jijini Addis Ababa- Ethiopia.
Mkutano wa AU katika Makao makuu ya Umoja huo Addis Ababa- Ethiopia uliofunguliwa leo hii eo Jijini Addis Ababa- Ethiopia ukiendelea

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...