THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN ATEMBELEA BANDA LA PROPERTY INTERNATIONAL, MAONYESHO YA SABASABA


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Property International, Abdul Haleem, kuhusu Ndege ya Kampuni hiyo inayopiga picha za juu kwa muda mfupi wakati wa upimaji wa Viwanja (Unmanned Ariel Vehcle As 1200) wakati Makamu wa Rais alipotembelea Banda la Maonyesho la Kampui hiyo kwenye Maonyesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, akisaini kitabu cha wageni wakati alipowasili kwenye Banda hilo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Property International, Abdul Haleem.


Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Property International, Abdul Haleem, akiendelea kutoa maelezo kwa Makamu wa Rais kuhusu ujenzi wa nyumba zinazojengwa na Kampuni hiyo ikiwa ni pamoja na kuuza na kukopesha Viwanja.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mtaalamu wa Teknolojia ya 'Mega Panel' wa Kampuni ya Property International, Jonathana Kibona, wakati alipotembelea Banda la maonyesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa la Kampuni hiyo ndani ya Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam, leo.