NA K-VIS BLOG/Khalfan Said

WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango,(pichani) amejiunga na Mfuko wa Pensheni wa PSPF, kupitia mpango wa uchangiaji wa hiari na kuhimiza wananchi kufanya hivyo kwani moja ya faida kubwa ni kujihakikishia kuwa na bima ya Afya.

Waziri aliyasema hayo leo Julai 8, 2017, wakati alipotembelea banda la PSPF lililoko jengo la Wizara ya Fedha na Mipango, kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere, maarufu Sabasabawakati wa Maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam yanayoendelea.

“Mimi nitoe wito kwa wananchi kujiunga zaidi na mpango huu kwani watafaidika na huduma ya afya na nyinyi muongeze kasi ya kutoa elimu kwa wananchi ili wajiunge zaidi.” Alisema Mhe. Dkt. Mpango.

Dkt. Mpango pia alikabidhiwa kadi yake ya uanachama muda mfupi baada ya kujiunga.

“Mheshimiwa Mpango wa Uchangiaji wa Hiari una faida nyingi na tumewalenga hasa watu wa kawaida kama vile wajasiriamali, wakulima, mama lishe, bodaboda, na machinga, na tumekuwa tukipata watu wengi wanaokuja kujisajili na Mpango huu na wengi wao wamevutiwa na hii Bima ya Afya ambayo ni moja ya faida azipatazo mwananchama” Alisema Afisa Uhusoano Mwandamizi wa PSPF, Bw. Abdul Njaidi wakati akimkabidhi Mhe. Waziri akdi yake ya uanachama.

Bw. Njaidi pia alimwambia Mhe. Waziri kuwa, kwa kujiunga kwake na Mpango huo wa uchangiaji wa Hiari, kutasaidia pia kuwakadia bima ya afya wasaidizi wake katika miradi kama vile ya shambani na ufugaji.

“ Hawa wote wanawezakuingia kwenye mpango huu wa bima kupitia uanachama wako katika Mfuko.” Alimuhakikishia Mhe. Waziri.


Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, (kulia), akikabidhiwa kadi ya uanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, kupitia Mpango wa Uchangiaji wa Hiari, (PSS), kutoka kwa Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo Bw. Abdul Njaidi, muda mfupi baada ya Mhe. Waziri kujiunga na Mpango huo leo Julai 8, 2017, kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere kunakofanyika Maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam, ambapo PSPF inatoa huduma zote kwenye Maonesho hayo.
Waziri Dkt. Mpango, (kulia), akimsikilizia kwa makini Bw. Njaidi kuhusu faida zitokanazo na kujiunga na Mpango wa PSS

Waziri Dkt. Mpango(kulia), akipokea fomu ya kujiunga na PSS, kutoka wka Balozi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Msanii maarufu, Mrisho Mpoto. Katikati ni Afisa Habari Mwanamizi wa PSPF, Bw. Abdul Njaidi.

Waziri Mpango (kulia), akiuliza maswali kwa maafisa wa PSPF.


HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...