Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) akimsalimia Mkuu wa Wilaya ya Kondoa, mkoani Dodoma, Sezaria Makota, mara baada ya kuwasili wilayani humo kwa ajili ya ziara ya kikazi. Wapili kulia ni Katibu Tawala wa Wilaya hiyo, Winnie Kitazi, na kulia ni Mkuu wa Jeshi la Polisi wilayani humo, SSP Mohamed Kitia.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) akiwasalimia Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama wa Wilaya ya Kondoa na Chemba mara baada ya kuwasili mjini Mkondoa kwa ajili ya ziara ya kikazi. 

 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati) akimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Kondoa, mkoani Dodoma, Sezaria Makota wakati alipokua akitoa taarifa yake ya Wilaya kwa kiongozi huyo ambaye yupo ziarani katika Wilaya ya Kondoa na Chemba. 
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati) akimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Chemba, mkoani Dodoma, Simon Odunga,wakati alipokua akitoa taarifa yake ya Wilaya kwa kiongozi huyo ambaye yupo ziarani katika Wilaya ya Kondoa na Chemba. 
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati) akimsikiliza Mkuu wa Jeshi la Polisi Wilaya ya Kondoa, SSP Mohamed Kitia wakati alipokua akitoa taarifa yake ya Ulinzi na Usalama wilayani humo. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kondoa, Sezaria Makota, na Mkuu wa Wilaya ya Chemba, Simon Odunga. Masauni yupo ziara ya kikazi katika Wilaya hizo ambapo alizitembelea Taasisi zilizopo ndani ya Wizara yake. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...