Na Felix Mwagara (MOHA) 
NAIBU Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni ameongozana na Mkuu wa Wilaya ya Muheza, Mkoani Tanga kufanya operesheni ya kuwasaka waharibifu  wa chanzo cha maji cha Mto Zigi ambao unapeleka maji Tanga mjini.
 Masauni alifika katika eneo hilo la tukio saa mbili usiku na kujionea maeneo yaliyoharibiwa kwa kuchimbwa mashimo makubwa na wahalifu hao wakidai kuwa wanatafuta madini ya dhahabu. Hata hivyo, hakuna mhalifu aliekamatwa katika eneo hilo wakati wa oparesheni hiyo. 
Akizungumza katika eneo hilo lililopo Tarafa ya Amani, wilayani humo jana, Masauni ambaye pia aliambatana na Mbunge wa Jimbo la Muheza, Balozi Adadi Rajabu, alisema Jeshi la Polisi litaendelea kufanya oparesheni katika eneo hilo usiku na mchana kwa kushirikiana na walinzi wa msitu  ili kuwaondoa wahalifu hao haraka iwezekanavyo. 
Masauni alisema licha ya Polisi kuendelea kufanya doria katika eneo hilo lakini wanatarajia kufungua kituo cha polisi ili kuongeza ulinzi zaidi katika eneo hilo muhimu ambalo ndio chanzo cha maji kwa sehemu kubwa ya wakazi wa Mji wa Tanga. 
“Tumepanga kuimarisha ulinzi zaidi katika eneo hili kwa kujenga kituo cha polisi ambapo askari wetu watashirikiana na walinzi wa misitu kufanya doria ya kupambana na wahalifu,” alisema Masauni na kuongeza;

“Kwa habari zisizo rasmi tulizozipata katika vyanzo vyetu, hawa wahalifu wanamtandao mkubwa wakishirikiana na watu mbalimbali wakiwemo wafanyabiashara na hata baadhi ya watumishi wa umma, tutaendelea kufanya uchunguzi huu kwa kina kwa kushirikiana na ofisi ya mkuu wa wilaya ili kuwabaini wahalifu wote haraka iwezekanavyo.”
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (aliyevaa Kaunda suti), akiongozwa na Afisa Tarafa ya Amani, wilayani Muheza, Ayubu Mhina kumuonyesha eneo la Kihara ambalo ni chanzo cha maji cha Mto Zigi ambalo linasambaza maji sehemu kubwa ya Jiji la Tanga ambalo limeharibiwa na wahalifu kwa kuchimba mashimo wakidai kuwa wanatafuta madini ya dhahabu. Hata hivyo, Jeshi la Polisi linafanya oparesheni katika eneo hilo mara kwa mara na pia linatarajia kujenga Kituo cha Polisi katika eneo hilo ili kupambana na wahalifu hao. Kushoto ni Mkuu wa Kituo cha Polisi Muheza, Oscar Joshua, na kulia ni Mshauri wa Wagambo wilayani humo.  
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto), akimsikiliza Mhifadhi Msaidizi Hifadhi ya Asili Amani, wilayani Muheza, Bob Matunda (wapili kushoto), alipokua anamuonyesha eneo la Kihara ambalo ni chanzo cha maji cha Mto Zigi lililoharibiwa na wahalifu kwa kuchimba mashimbo wakidai wanatafuta madini ya dhahabu katika eneo hilo. Masauni aliongozana na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya muda wa usiku kwenda kuangalia waharibifu hao walivyoliharibu eneo hilo.  
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akimfafanulia jambo Mkuu wa Wilaya ya Muheza, Mhandisi Mwanaasha Tumbo (kulia), mara baada ya kuangalia eneo la chanzo cha maji katika hifadhi ya Msitu wa Asili wa Amani ambalo liliharibiwa na wahalifu kwa kuchimba mashimo katika eneo la Kihara ambalo ni chanzo cha maji, wakidai wanatafuta madini ya dhahabu katika eneo hilo.  Masauni akiongozana na Mkuu wa Wilaya hiyo, walifika eneo hilo la tukio muda wa usiku.  Katikati ni Afisa Tarafa ya Amani, wilayani Muheza, Ayubu Mhina. 
Mbunge wa Jimbo Muheza, Balozi Adadi Rajabu akimuonyesha  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto), ameneo mbalimbali yaliyoathiriwa na wachimbaji wa madini katika eneo hilo ambalo ni muhimu kutokana kuwa na chanzo cha maji ambayo yanatumika katika eneo kubwa mkoani Tanga. Wapili kushoto ni Mkuu wa Wilaya hiyo, Mwanaasha Tumbo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Kwa taarifa kamili BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...